Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

13 Septemba 2019

13 Septemba 2019

Pakua

Katika jarida la kina leo hii Flora Nducha anakuletea

-Kenya imezindua rasmi chanjo ya kwanza ya malaria iliyo kwenye majaribio, ugonjwa ambao hukatili maisha ya maelfu ya watu kila mwaka.

-Shirika la elimu sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO limeonya kwamba hatua za haraka zisipochukuliwa watoto milioni 12 hawatowahi kuonja shule ifikapo 2030

-Shirika la afya duniani WHO kwa kushirikiana na mamlaka ya afya nchini Tanzania wamesema hii leo kuwa wanapeleka timu ya wataalamu nchini humo kuchunguza fununu za kifo kutokana na ugonjwa ambao haujajulikana bado.

-Mada kwa kina utamsikia kijana Isaya Yunge kutoka Tanzania aliyeanzisha spika janja "Kaya" akitoa ushauri kwa Afrika kuanza mchakato wa kukusanya takwimu zao wenyewe

-Neno la wiki jumahili tunaangazia jinsi lugha ya Kiswahili inavyozidi kupasua anga za kimataifa na kukua.

Audio Credit
UN News/Flora Nducha
Audio Duration
10'47"