Sauti Mpya

20 Agosti 2019

Je wafahamu kuwa mwanamke mmoja raia wa Cameroon alilazimika kuwavisha wanae wa kiume hijab na sketi ili wasichukuliwe na magaidi wa Boko Haram? Pata basi kisa hiki kwenye jarida letu la leo sambamba na taarifa kutoka Libya kuhusu mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kwenye mji wa kusini wa Murzuq.

Sauti -
11'49"

Huduma ya kibinadamu ni wito-Wakili Kamunya

Kutoa huduma ya kibinadamu iwe ni katika mazingira yoyote yale ni wito ambao ni lazima utoke moyoni amesema Ann N.

Sauti -
6'8"

Kutoka kuwa mtangazaji hadi mhudumu wa kibinadamu

Nchini Uganda mtangazaji wa kipindi cha masuala ya kijamii mjini Hoima ameleta nuru kwa watoto wengi waliohatarini baada ya kuanzisha kituo cha kulea watoto wakiwemo yatima na wanaozaliwa na watu wenye matatizo ya akili. Je, mwanahabari huyo amegeukaje kuwa mhudumu wa kibinadamu?

Sauti -
2'43"

Tunalenga kuleta mabadiliko pia DRC- Dkt. Mvumbi

Katika kuadhimisha siku hii ya kimataifa ya huduma za kibinadamu , moja ya nchi ambayo inahitaji kwa hali na mali huduma hizo ni Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC, ambayo imeghubikwa na mjangamakubwa matano , kipindupindu, njaa, kutokuwa na uhakika wa chakula, vita nae bola.

Sauti -
2'19"

Wanawake wahudumu wa kibinadamu wako mstari wa mbele kutoa huduma-Guterres

Leo ni siku ya huduma za kibinadamu duniani ambapo Umoja wa Mataifa unapigia chepuo mwaka huu wanawake waliojikita katika kutoa huduma za kibinadamu kote ulimwenguni.

Sauti -
1'55"

19 Agosti 2019

Hii leo ni siku ya huduma za kibinadamu duniani na Grace Kaneiya anakuletea ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, maudhui ya siku yakiwa ni wanawake wanaotoa huduma za kibinadamu.

Sauti -
14'

Neno la Wiki- "Wame"

Leo katika Neno la Wiki tunakwenda kwa mtaalam wetu wa kiswahili juma hili ambaye ni Mwanahija Ali Juma katibu mtendaji wa Baraza la Kiswahili Zanzibar , BAKIZA anafafanua matumizi ya neno “WAME” katika sentensi yenye nomino mbili.

 

 

 

 

 

Sauti -
1'12"

Elimu kwa watoto warohingya bado ni ndoto-UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema miaka miwili ya harakati za kila uchao za kujikwamua kimaisha kwa warohingya waliosaka hifadhi nchini Bangladesh zimetumbukiza nyongo mustakabali wa elimu kwa kizazi kizima

Sauti -
2'21"

Nchini Burundi kampeni ya chanjo dhidi ya ebola inaendelea-WHO

Maandalizi na kampeni ya chanjo dhidi ya Ebola kwa mataifa jirani na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ambako ugonjwa huo bado unaendelea ni muhimu limesema shirika la afya duniani WHO. 

Sauti -
2'15"