Sauti Mpya

Kuelekea ICPD 25, Zimbabwe yachukua hatua madhubuti kunusuru vifo vya wanawake na watoto wa kike

Miaka 25 iliyopita huko Cairo Misri nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa waliazimia kupunguza na hatimaye kutokomeza vifo vya wanawake, wajawazito, watoto wachanga na watoto ili hatimaye dunia hii iwe na ustawi kwa wote bila kujali mtu anaishi eneo gani.

Sauti -
3'30"

Nimejitolea kukomesha ajira kwa watoto Uganda sababu nimeipitia asema Namirembe

Wahenga walisema siri ya mtungi aijuaye kata na uchungu wa ajira ya mtoto anaujua mtoto aliyeipitia, kauli hiyo imetolewa na Molly Namirembe mwanaharakati wa kupambana na ajira ya watoto nchini Uganda ambaye yeye mwenyewe alipitia madhila hayo na jinamizi lake linamtesa hadi sasa.

Sauti -
1'43"

Mtoto mkimbizi Gift Maliamungu aazimia kuendelea na masomo yangu hadi Chuo Kikuu kama Mungu ataruhusu

Gift mtoto aliyejikuta peke yake nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC baada ya kuyakimbia mapigano nchini Sudan Kusini, amefanya vizuri katika mtihani wa darasa la sita baada ya kuibuka na alama za juu katika mashindano ya tahajia za maneno lakini matarajio yake ya kuendelea na masomo ya

Sauti -
2'47"

Upofu unaokabili watu bilioni 1 ungaliweza kuepukwa iwapo wangalipata tiba yasema WHO

Takribani watu bilioni 2.2 duniani kote wana uoni hafifu au upofu, kutokana na ukosefu wa huduma bora za afya, limesema shirika la afya duniani hii leo katika ripoti yake ya kwanza kuhusu hali ya uoni duniani.

Sauti -
2'50"

08 Oktoba 2019

Je wafahamu kuwa watu bilioni 2.2 wanapata upofu au uoni hafifu ilhali wanaweza kuepuka shida hiyo? Ni miongoni tu mwa habari zetu za leo kwenye Jarida la Habari za UN likiletwa kwako na Flora Nducha.

Sauti -
13'2"

Wanawake wa Mazingira Women Initiative wakijikita katika kuboresha makazi yao Kibera Kenya

Wakati ulimwengu unaadhimisha siku ya makazi duniani bado mamilioni ya watu wanaishi katika mazingira duni hususan kwenye nchi zinazoendela. Katika mitaa ya mabanda kwa kiwango kikubwa mazingira huwa duni sana.

Sauti -
4'11"

MINUSCA ni mkombozi mkubwa kwa wakimbizi CAR

Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu nchini humo,

Sauti -
1'40"

Sitachoka kuelimisha viongozi wa kesho popote nilipo:Mwalimu Reath

Ualimu ukiwa ni wito wako popote utafundisha , hiyo ni kauli ya mkimbizi kutoka Sudan Kusini ambaye pia ni mwalimu kwa sasa yuko ukimbizini nchini Ethiopia anakoendeleza wito wake wa ualimu kwa watoto wakimbizi. Amina Hassan na taarifa zaidi

Sauti -
2'14"

Kushughulikia tatizo la utaifa kusiwanyime haki zaidi wakimbizi:Grandi

Suala la ulinzi wa wakimbizi ni moja ya vipaumbele vya awali kabisa vya Umoja wa Mataifa takriban miongo saba iliyopita hata hivyo, ufurushwaji wa watu bado unazua wasiwasi mkubwa kimataifa. Taarifa kamili na Arnold Kayanda

Sauti -
2'24"

07 Oktoba 2019

Hii leo jaridani na Flora Nducha anaanzia Geneva Uswisi ambako suala la wakimbizi lajadiliwa na UNHCR yahoji mpaka lini wakimbizi watak

Sauti -
12'7"