Kashfa za ukatili wa kingono zinapungua- Lacroix
Mwaka 2017 ulikuwa wa majonzi makubwa kwenye operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa.
Mwaka 2017 ulikuwa wa majonzi makubwa kwenye operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa.
Wanamgambo wa kabila la watwa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC wamesalimisha mishale 3,000.
Mishale hiyo ilikuwa inatumika kwenye mapigano ya kikabila kati yao ya na jamii wa kabila la wabantu kwenye eneo la Manono lililopo jimbo la Tanganyika.
Katika ajenda ya maendeleo endelevu SDGs ya mwaka 2030, lengo namba 3 la afya bora kwa kila mtu, limekuwa changamoto kubwa sana hasa kwa nchi za Afrika zilizoko kusini mwa jangwa la sahara.
Duru ya pili ya uchaguzi nchini Liberia imefanyika hapo jana.
Bajeti ya umoja wa Mataifa kwa mwaka 2018-2019 yenye kurasa zaidi ya elfu 8 zilizosheheni maelezo ya mipango mbalimbali na takwimu za taasisi hii kubwa zaidi duniani ilipitishwa mwishoni mwa juma na nchi 193 wanachama wa Umoja huo ikiwa na upungufu wa mamilioni ya dola ikilinganishwa na mwaka 201
Harakati za kuhamisha kutoka Libya wakimbizi walio hatarini zaidi zinaendelea chini ya usimamizi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR.
Katika hatua ya hivi karibuni zaidi wakimbizi 162 walisafirishwa kwenye Roma, Italia kwa kutumia ndege mbili.
Esther, mwenye umri wa miaka 25 aliishi kwa amani na furaha na familia yake huko Kasai, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, lakini ghafla akajikutaka akilazimika kuacha kila kitu chake na kukimbilia yeye na familia yake nchini Angola. Kulikoni? Assumpta Massoi na maelezo zaidi.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amekaribisha hatua iliyofikiwa huko Jamhuri ya Congo baada ya serikali na Frédéric Bintsamou ambaye hujulikana zaidi kama mchungaji Ntumi kutia saini makubaliano ya kusitisha chuki kati yao.
Nchini Papua New Guinea, wanawake wamechukua hatua kulinda afya zao. Baada ya safari za kutwa kucha kufuata vituo vya afya vilivyokuwa vinapatikana umbali mrefu, wanawake walishikamana na kusaka usaidizi kutoka Benki ya Dunia ili kuanzisha kituo cha afya kwenye kijiji chao.
Mkuu wa operesheni za amani mashinani kwenye Umoja wa Mataifa Atul Khare amesema mradi wa pande tatu unaohusisha Japan, Afrika na Umoja wa Mataifa umezaa matunda katika kuimarisha operesheni za ulinzi wa amani.