Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

25 JULAI 2024

25 JULAI 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoangazia siku ya kimataifa ya kuzuia watu  kuzama majini na tunakupeleka nchini Tanzania kufuatilia suala hili. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo za Ethiopia, Bangladesh kusini mwa Afrika. Pia tunakuletea ufafanuzi wa msemo “Lakupita lapishwa.”

  1. Idadi ya watu Ethiopia waliokufa baada ya matukio matatu ya maporomoko ya udongo kusini mwa Ethiopia yaliyochochewa na mvua kubwa imeongezeka na kufikia 257 jana Jumatano huku idadi ikitarajiwa kufikia 500, na kwamba watu zaidi ya 15,000 wanatakiwa kuhamishwa. Imesema Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA.
  2. Maandamano ya kupinga serikali yakiendelea nchini Bangladesh ambako zaidi ya watu 160 wakiwemo polisi wameripotiwa kuuawa, wataalamu wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu wameitaka serikali ya Bangladesh iache mara moja msako dhidi ya waandamanaji na wapinzaji wa kisiasa, irejeshe mtandao wa intaneti na iwajibike na ukiukwaji wa haki za binadamu.
  3. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema ukame mkali unaokumba eneo la kusini mwa Afrika unatishia mamia ya maelfu ya watoto kwenye nchi sita zilizoathiriwa vibaya zaidi na ukame kukabiliwa na utapiamlo uliokithiri. Nchi hizo ambazo zimetangaza janga la uhaba wa chakula kitaifa kutokana na ukame ni Lesotho, Botswana, Malawi, Namibia, Zambia na Zimbabwe.
  4. Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, Mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia maana ya methali “Lakupita lapishwa.”

Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 

Audio Credit
Flora Nducha
Sauti
9'56"