Kuhusu sisi

Radio ya Umoja wa Mataifa inatangaza habari kila siku kwa lugha ya Kiswahili, Kiarabu, Kichina, Kiingereza, Kifaransa, Kireno, Kirusi na Kihispania. Na mara moja kwa wiki inakuwa na vipindi vya lugha ya Creole cha kifaransa, Kibengali, Kihindi, Kiurdu na kiindonesia.

Radio ya UM inabadilisha taarifa zake kutokana na habari mpya zinavyokuja kila mara kwa siku. Pia inaandaa makala na kufanya uchambuzi wa mada mbalimbali za kijamii, kisiasa, kiuchumi, maendeleo na masuala yanayohusu tamaduni zinazohusisha Umoja wa Mataifa na kazi zake. Vipindi vya Radio ya UM viko vingi ni kuanzia Taarifa za habari, makala, vipindi maalumu na taarifa za habari za kila siku na zile za kila wiki.

Na vipindi vyote hivyo vinaweza kutumiwa na vyombo vingine vya habari au watangazaji, na vinaweza kutumiwa kama chanzo cha habari kwa waandishi binafsi.Na kwa kuongezea tuu ni kwamba vipindi vyote hivyo na sauti zingine kwenye tovuti yetu vinatolewa bure bila malipo yoyote