Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

26 Julai 2024

26 Julai 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia ufunguzi wa michezo ya Olimpiki na Jitihada za pamoja za kukabiliana na changamoto za afya ya umma barani Afrika. Makala tutasalia nchini Paris katika michezo ya Olimpiki na mashinani tunasikia mafunzo kushusu ulemavu wa kutosikia. 

  1. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ambaye yuko Paris Ufaransa kuhudhuria ufunguzi wa michezo ya Olimpiki ya majira ya joto mwaka 2024 amezungumza katika mkutano na waandishi wa habari akiwa pamoja na Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki Thomas Bach na kuipongeza kamati hiyo kwa kuendelea kuwajumuisha wakimbizi wanamichezo.
  2. Jitihada za pamoja za kukabiliana na changamoto za afya ya umma zinazidi kuboresha upatikanaji na utoaji wa huduma za afya. Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni, WHO kanda ya Afrika kwa kushirikiana na nchi wanachama na washirika wake linaendelea kutimiza ajenda yake ya mabadiliko ili kuimarisha mifumo ya afya na kuongeza misaada kwa nchi katika ukanda wa Afrika.
  3. Makala inamulika mmoja wa wanariadha wanaowakilisha timu ya wakimbizi kwenye michezo ya olimpiki iliyoanza leo Paris, Ufaransa. Safari yake na matumaini yake akilenga kukimbia mbio za mita 800 kwa dakika 2 na sekunde 10 badala ya dakika 2 na sekunde 12.
  4. Na mashinani Dkt. Kaitesi Batamuliza Mukara, Mshauri wa masuala ya masikio, kusikia na uangalizi wa macho kutoka Ofisi ya kikanda barani Afrika ya Shirika la Afya Duniani, WHO akieleza juhudi za shirika hilo za kusaidia watu wenye changamoto ya kusikia.

Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu! 

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
10'