31 DESEMBA 2020
Katika Jarida la Umoja wa Mataifa hii leo Anold Kayanda anakuletea salamu za mwisho wa mwaka kutoka kwa wafanyakazi
-Wanazungumzia mambo mbalimbali ikiwemo malengo ya maendeleo endelevu SDGs
-Je mwaka 2020 umekuwaje?
Katika Jarida la Umoja wa Mataifa hii leo Anold Kayanda anakuletea salamu za mwisho wa mwaka kutoka kwa wafanyakazi
-Wanazungumzia mambo mbalimbali ikiwemo malengo ya maendeleo endelevu SDGs
-Je mwaka 2020 umekuwaje?
Mwaka 2020 umekuwa wenye changamoto nyingi zilizoathiri watu wa tabaka mbalimbali ingawa kwa viwango tofauti.
Katika Jarida la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea matukio ya mwaka 2020
-Mwaka 2020 ulitangazwa kuwa mwaka wa wauguzi na wakunga na shirika la afya duniani WHO
Nchini Tanzania shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) kwa kushirikiana na serikali na wadau wake wameandaa mpango wa miaka mitano wenye lengo la kuoanisha shughuli za kilimo na lishe ili kukabiliana na utapiamlo.
Katika Jarida la Habari za Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF , nchini Kenya, limegawa redio 10,000 zinazotumia nishati ya sola kwa kaya masikini nchini humo ili watoto wengi wapate fursa ya kusoma nyumbani wakati huu wakijianda kurejea shuleni. Tupate maelezo zaidi na Jason Nyakundi
Karika jarida la mada kwa kina hii leo Flora Nducha anakuletea
Maji ni hai ni kauli ambayo imethibitika kwa wakazi wa jimbo la Dankpen nchini Togo, baada ya Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la chakula na kilimo, FAO na serikali, kukarabati bwawa linalotumika hivi sasa kwa shughuli siyo tu za umwagiliaji, bali pia maji kwa wanyama na utalii.
Nchini Senegal, wakulima na wafanyabiashara wadogo wameushukuru mradi wa kusaidia maendeleo ya sekta ya kilimo, PAFA, unaofadhiliwa na Mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo IFAD. Anold Kayanda na maelezo zaidi.
(TAARIFA YA ANOLD KAYANDA)