Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viazi lishe vimetukomboa na mafunzo ya FAO yametuimarisha

Viazi lishe vimetukomboa na mafunzo ya FAO yametuimarisha

Pakua

Nchini Tanzania, hususan mkoa wa Singida ulioko katikati kwa taifa hilo la Afrika Mashariki, shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO linaendelea na harakati zake za kuhakikisha taifa hilo la Afrika Mashariki linafanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs, likiwemo lile la kwanza la kutokomeza njaa na la pili la kutokomeza umaskini yanafikiwa. Miongoni mwa harakati za karibuni ni mradi wa pamoja wa kuongeza kasi ya uwezeshaji wanawake kiuchumi vijijini unaotekelezwa wilaya ya Ikungi, mkoani humo ambapo wanaume wanashirikiana pia na wake zao kwenye shughuli za kilimo shambani. Makala ya leo imemmulika mmoja wa wanaume hao akiwa shambani mwake,  huku Afisa ugani wilayani Ikungi akifafanua utekelezaji wa mradi huo.

Audio Credit
Bosco Vincent/Assumpta Massoi
Audio Duration
3'47"
Photo Credit
UN News