Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kikosi maalumu cha UNAMID Jeber Mara kujumuisha Watanzania:Ngodi

Walinda amani wa UM wapiga doria Darfur Sudan. Picha: UNAMID

Kikosi maalumu cha UNAMID Jeber Mara kujumuisha Watanzania:Ngodi

Kikosi maalumu cha mpango wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika wa kulinda Amani jimboni Darfur nchini Sudan UNAMID kitakachohudumu  katika safu za milima ya Jaber Mara eneo ambalo ni vigumu kufikika nchini humo , kitajumuisha walinda amani kutoka Tanzania. Taarifa zaidi na Selina Jerobon

(TAARIFA YA SELINA)

Hayo ni kwa mujibu wa mkuu wa majeshi ya ulinzi ya UNAMID Luteni Jenerali Leonard Ngondi wakati wa ziara yake inayokamilika leo katika kambi za Khorabeche na Minawashe zinazokaliwa na wanajeshi kutoka na Tanzania akiwataka kujiandaa kwa ajili ya operesheni hiyo.

Ameongeza kuwa kinachosubiriwa sasa ni tamko la baraza la usalama kutoa mwelekezo wa utekelezaji wa awamu ya pili ya upunguzaji wa idadi ya vikosi vya walinda Amani baada ya awamu ya kwanza iliyoondoa vikosi vitatu kukamilika

(SAUTI YA LUTENI JENERALI LEONARD NGONDI -CUT 1)

Amesema ana imani na wanajeshi hao kutoka Tanzania kwamba wataipeperusha vyema bendera ya UNAMID na nchi yao, akisisitiza wajibu wao katika operesheni hiyo sio ya mapigano, bali yatafanyika pale inapobidi kujilinda na yeyote atakayehatarisha usalama wa Umoja wa Mataifa na mali za Umoja wa Mataifa. 

(SAUTI YA LUTENI JENERALI LEONARD NGONDI-CUT 2) 

Safu za milima ya Jaber Mara imekuwa vigumu kufikika kwa muda mrefu kutokana na miundombinu mibovu na kukaliwa na waasi.