Chad: Operesheni za WFP ziko hatarini kusitishwa
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) leo limeonya kuhusu uwezekano wa kusitishwa kwa msaada wake wa chakula na lishe kwa watu milioni 1.4 walioathiriwa na mgogoro nchini Chad - ikiwa ni pamoja na wakimbizi wapya wa Sudan waliowasili - kutokana na vikwazo vya fedha.