Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Sudan

13 NOVEMBA 2025

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoangazia simulizi za waahirika wa Kimbunga Melissaikiwa ni wiki ya pili sasa baada ya kupiga magharibi mwa Jamaica, na kuacha zahma kubwa kwa wakaazi. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na jifunze Kiswahili.

Sauti
10'40"

03 NOVEMBA 2025

Hii leo jaridani tunaangazia hali ya haki za binadamu nchini Sudan, Mpango wa Ufadhili Wajasiriamali Wanawake, (We-Fi) nchini Tanzania, na kilimo ni moja ya sekta muhimu za kiuchumi nchini Nigeria.

Sauti
9'50"
© UNICEF/Mohammed Jamal

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC yaeleza wasiwasi mkubwa kuhusu mauaji na uhalifu El Fasher

Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imetoa tamko juu ya wasiwasi mkubwa kufuatia ripoti mpya kutoka El-Fasher, jimboni Darfur Kaskazini, nchini Sudan, zikieleza kuwepo kwa mauaji ya halaiki, ubakaji, na uhalifu mwingine unaodaiwa kufanywa wakati wa mashambulizi ya Vikosi vya Usaidizi wa Haraka (RSF). Taarifa zaidi na Sheilah Jepngetich.

Sauti
2'37"
Familia ambazo zilikimbia mapigano huko Zamzam na El Fasher huko Darfur Kaskazini, zinatafuta hifadhi huko Tawila.
© UNICEF/Mohammed Jamal

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) yaeleza wasiwasi mkubwa kuhusu mauaji na uhalifu El Fasher

Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imetoa tamko juu ya wasiwasi mkubwa kufuatia ripoti mpya kutoka El-Fasher, jimboni Darfur Kaskazini, nchini Sudan, zikieleza kuwepo kwa mauaji ya halaiki, ubakaji, na uhalifu mwingine unaodaiwa kufanywa wakati wa mashambulizi ya Vikosi vya Usaidizi wa Haraka (RSF). 

Sauti
2'37"
Mwanamke akiitayarishia familia yake chakula huko El Fasher, Darfur Kaskazini ambako watu wamenaswa kutokana na mapigano
© UNICEF

Utekaji nyara, mauaji ya halaiki na ubakaji Sudan: UN yatahadharisha ukatili El-Fasher

Tangu kuanguka kwa jiji la El-Fasher mikononi mwa Rapid Support Forces (RSFambavyo ni vikosi vya waasi vya Sudan, maelfu ya raia wamekimbia jiji hilo. Wote wameripoti ukiukwaji wa haki za binadamu unaoendelea katika eneo hilo, kwa mujibu wa Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa (OHCHR), ambayo imetahadharisha kuwa kuna taarifa mpya zinazoendelea  kujitokeza kuhusu ukatili uliofanywa wakati na baada ya kuanguka kwa jiji hilo la Darfur Kaskazini.