Guterres kushiriki mkutano wa AU-EU Abidjan

28 Novemba 2017

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amezungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya umoja huo jijini New York, Marekani akiangazia masuala muhimu ya chombo hicho.

Miongoni mwao mambo hayo ni ziara ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko Abidjan nchini Côte d'Ivoire ambako anawasili leo tayari kuhutubia mkutano wa tano wa ushirikiano wa nchi za Muungano wa Afrika, AU na Muungano wa Ulaya, EU.

Maudhui ya mkutano huo ni kuwekeza kwa vijana kwa ajili ya mustakhbali bora.

image
Opresheni MINUSMA. Picha: MINUSMA

Halikadhalika Bwana Dujarric amezungumzia hali ya amani na usalama huko Mali ambako leo ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, MINUSCA umesema..(Sauti ya Stephane Dujarric)

“Wameripoti mashambulizi manne kwenye mji wa Kidal hii leo. Kambi tatu tofauti zilishambulia kwa makombora na roketi. Operesheni za msako zinaendelea. Ujumbe huo wa kulinda amani pia umeripoti kuwa leo asubuhi walinda amani waliokuwa kwenye doria walishambuliwa lakini hakuna aliyejeruhiwa. Tumekuwa tunalaani vitendo hivi ambavyo vinaweza kuwa uhalifu wa kivita kwa mujibu wa sheria za kimataifa.”

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter