Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chondechonde wahisani wakimbizi wa Somalia bado wanawahitaji: Grandi

Kamishina mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR bwana Filipo Grandi ziarani Kenya. Picha: UNHCR/Video capture

Chondechonde wahisani wakimbizi wa Somalia bado wanawahitaji: Grandi

Kamishina mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR bwana Filipo Grandi ametoa wito wa usaidizi zaidi kwa wakimbizi wa Somalia walioko nchini Kenya. Flora Nducha na taarifa kamili

(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)

NATTS……

Akiwa ziarani katika moja ya kambi kubwa zaidi na ya zamani sana ya wakimbizi duniani ya Dadaab, Grandi amekutana na wakimbizi wa Kisomali waliochagua kurejea nyumbani na wengine wengi wanaosalia kambini hapo hadi pale usalama utakapotengamaa kabisa nchini Somalia. Kuna wakimbizi zaidi ya 400,000 wanaoishi kwenye kambi ya Dadaab na asilimia kubwa ni Wasomali.

Bwana Grandi ametoa wito wa msaada wa kimataifa na fedha kwa ajilia ya wakimbizi wa Kisomali wanaorejea nyumbani kwa hiyari na wale wanaosalia kambini Kenya akisema mahitaji yao ni mengi na UNHCR haina fedha za kukidhi mahitaji hayo yote.

(SAUTI YA FILIPPO GRANDI)

“Ombi letu kwa wahisani ni kutokana tamaa sasa kwa ajili ya Dadaab. Kambi hii, na watu wanaoishi humu wataendelea kuhitaji msaada hata kama kuna uwezekano wa kuhamishwa. Watu wengi hawataki kuchukua fursa hizo kwa sasa, na ni lazima wawe na uhuru wa kutozichukua fursa hizo na waendelee kulindwa na kupatiwa usaidizi hapa.”

Kenya ikiwa ni hitimisho la ziara yake ya siku tantu Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika, Grandi alipata fursa pia ya kuzungumza na viongozi wa serikali akiwemo Rais Uhuru Kenyata ambaye amemshukuru sana kwa kuendelea kuhifadhi idadi kubwa ya wakimbizi kutoka sehemu mbalimbali.