Kundi la wakimbizi 76 kutoka Ethiopia waliokuwa wanaishi kwenye kambi ya Kakuma nchini Kenya wamerejea nyumbani ikiwa ni mara ya kwanza ya utekelezaji wa mpango wa kurejea nyumbani kwa hiari kwa wakimbizi hao wa Ethiopia.
Maelfu ya wakimbizi wa Somalia walioko katika kambi za wakimbizi za Dadaanb na Kakuma nchini Kenya wanakata shauri na kuamua kurejea nyumbani wakiwa na matumaini ya kupata kazi na Maisha bora . Jason Nyakundi na taarifa zaidi
Maryan Mohamed, mkimbizi kutoka Somalia anayeishi kambini Daadab nchini Kenya ameongoza kwa kupata alama za juu kuliko wanafunzi wenzake kwenye mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi, KCPE, kwa mwaka huu wa 2018.
Katika tamasha la Muziki lililoleta pamoja washiriki zaidi ya 20 kutoka kambi ya Wakimbizi ya Kakuma na Dadaab, pamoja na wanamuziki wengine kutoka mji mkuu Nairobi nchini Kenya, tunamulika ujasiri wa Mwanamuziki Ali Doze, Msanii ambaye ni mmoja wa wakimbizi katika kambi ya Dadaab nchini Kenya.