Lacroix awajulia hali majeruhi wa Tanzania waliolazwa Uganda

13 Disemba 2017

Mkuu wa operesheni za ulinzi za Umoja wa Mataifa Jean-Pierre Lacroix amewajulia hali walinda amani wawili wa Tanzania waliolazwa katika hospital ya Mulago mjini Kampala nchini Uganda.

Walinda amani hao wanapatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa wakati wa shambulio huko Semuliki, Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC Alhamisi ya wiki iliyopita.

Mkuu wa operesheni za ulinzi za Umoja wa Mataifa Jean-Pierre Lacroix awajulia hali walinda amani wawili wa Tanzania waliolazwa katika hospital ya Mulago mjini Kampala nchini Uganda. Picha: UM

Akiwa wodini kuzungumza na majeruhi hao kuwajulia hali, mmoja wao amesema..

(Nats)

Na ndipo Bwana Lacroix akasema..

Mkuu wa operesheni za ulinzi za Umoja wa Mataifa Jean-Pierre Lacroix awajulia hali walinda amani wawili wa Tanzania waliolazwa katika hospital ya Mulago mjini Kampala nchini Uganda. Picha: UM

(Sauti ya Jean-Pierre Lacroix)

« Nimetoka idara ya ulinzi wa amani ya Umoja wa Mataifa, New York, nimekuja kuwajulia hali na kusema asante sana kwa huduma yenu. Nakutakia kila la kheri. »

Baada  ya kutoka Mulago nchini Uganda, Bwana Lacroix ameelekea jijini Dar es salaam nchini Tanzania ambako kesho atahudhuria tukio maalum la kuaga miili ya walinda amani 14 waliouawa huko DRC.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter