Changamoto ya ufadhili yalazimisha kupunguzwa kwa shughuli za ulinzi wa amani za UN
Ukosefu mkubwa wa fedha unatishia kulemaza shughuli za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa duniani kote, huku shirika hilo likionya kuwa litalazimika kupunguza doria, kufunga ofisi za mashinani, na kuwarejesha maelfu ya walinda amani kutokana na ucheleweshaji wa malipo kutoka kwa nchi wanachama.