Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres alaani vikali DPRK kwa kurusha kombora

jaribio la kombora kutoka DPRK. Picha: UM/Idhaa ya Kiswahili

Guterres alaani vikali DPRK kwa kurusha kombora

Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Korea, DPRK ijulikanayo pia kama Korea Kaskazini imefanya jaribio jingine la kombora la masafa marefu usiku wa kuamkia leo.

Kufuatia kitendo hicho, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani vikali kitendo hicho akisema ni kiashiria dhahiri cha nchi hiyo kukiuka maazimio ya Baraza la Usalama la umoja huo.

Kupitia taarifa ya msemaji wake, Guterres amesema kitendo hicho pia ni kinyume na mtazamo wa pamoja wa jumuiya ya kimataifa.

Katibu Mkuu ameisihi DPRK ijizue kufanya vitendo zaidi ambavyo vinatishia zaidi amani huku akisisitiza azma yake ya kushirkiana na pande zote husika kupunguza mvutano kutokana na kitendo hicho cha leo.