Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuache fikra potofu tunapojadili uhamiaji- Guterres

Wahamiaji wakiwa huko Berlin nchini Ujerumani wakisubiri kusajiliwa. (Picha:UNICEF/Ashley Gilbertson VII)

Tuache fikra potofu tunapojadili uhamiaji- Guterres

Amani na Usalama

Mtazamo potofu kuhusu uhamiaji na wahamiaji umeendelea kukwamisha matumizi bora ya dhana hiyo kote ulimwenguni, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo wakati akizindua ripoti yake kuhusu mbinu za kufanya uhamiaji uwe na manufaa kwa wote. Patrick Newman na ripoti kamili.

(Taarifa ya Patrick Newman)

Katika ripoti yake Bwana Guterres amesema licha ya mchango chanya wa wahamiaji kwenye uchumi wa nchi wanamoishi au katika nchi walimotoka.

Mathalani amesema wahamiaji wanachangia kwenye maendeleo ya kimataifa kwa kazi zao na pia kwa fedha wanazotuma kule wanakotoka.

Ametolea mfano mwaka jana pekee akisema wahamiaji walituma karibu dola bilioni 600, kiwango ambacho ni mara tatu zaidi ya fedha za usaidizi wa maendeleo.

Licha ya mchango huo..

image
Hapa ni Uturuki, wanaume hawa wahamiaji kutoka Syria wakijifunza ushoni kama njia mojawapo ya kujipatia kipato. (Picha:© IOM/ Muse Mohammed)
(Sauti ya Antonio Guterres)

“Bado uhamiaji ni chanzo cha mvutano wa kisiasa na majanga ya kibinadamu. Idadi kubwa ya wahamiaji wanaishi na kufanya kazi kinyume cha sheria. Wanaohaha zaidi wanaweka maisha yao hatarini kuingia nchi ambako wanakumbwa na shuku na manyanyaso.”

Bwana Guterres amesema matokeo yake kuna ongezeko la kutokuwa na imani na sera zinazolenga kudhibiti harakati za uhamiaji za binadamu.

Kwa mantiki hiyo Katibu Mkuu amesema ripoti yake…

(Sauti ya António  Guterres)

“Natoa wito kwetu sisi kujikita katika mambo muhimu chanya ya uhamiaji na kutumia ushuhuda dhahiri badala ya fikra zisizo sahihi kama msingi wa kukabiliana na changamoto za uhamiaji. Na zaidi ya yote nasihi mwenendo wenye utu ambao unaweka ubinadamu wetu kama kitovu cha mjadala.”