Miaka mitatu ya kambi ya Zaatari,bado changamoto kubwa:UNHCR

28 Julai 2015

Leo ni miaka miaka mitatatu tangu kufungunguliwa kwa kambi ya wakimbizi ya Zaatari huko Jordan ambayo ndio iliyo kubwa zaidi Mashariki ya Kati. Kambi hiyo ilijengwa kwa siku tisa tu kukabiliana na idaidi kubwa ya wakimbizi wanaomiminika nchini Syria.

Hivi leo Zaatari ni makaazi ya takriban wakimbizi 81,000 na idadi hiyo inazidi kuogozeka kila uchao. Ariane Rummery ni msemaji wa Shirika la kuhudumia wakimbizi, UNHCR na hapa anaelezea changamoto zinazokumba shirika hilo..

(Sauti ya Arriane)

“Zaidi ya nusu ya idadi ya wakimbizi ni watoto na changamoto ni jinsi gani tunaweza kuendeleza masomo yaliyovurugika vibaya wakati wa mapigano. Mmoja kati ya watoto watatu ndani ya kambi ya Zaatari hawaendi shule rasmi au isiyo rasmi ni lazima tutafute mbinu zaidi kwa kizazi hiki hapa na wengine zaidi duniani kote ambao ni mustakabali wa Syria.”

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter