Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama lajadili tishio la Boko Haram

Baraza la usalama lajadili tishio la Boko Haram

Baraza la Usalama leo limekutana kujadili masuala mbalimbali ya amani na usalama ikiwamo vitisho vya ugaidi kupitia kundi la Boko Haram lilikojikita Afrika Magharibi hususani Nigeria ambapo kikao hicho kimepitisha tamko la Rais wa baraza na  Kikundi kazi cha kimataifa maalum kwa ajili ya kupambana na Boko Haram.

Akiongea katika mkutano huo mwakilishi wa kudumu wa Chad katika Umoja wa Mataifa Mahamat Zene Cherif ambaye nchi yake imeungana na Nigeria katika mapambano dhidi ya Boko Haram ameliambia baraza la usalama kuwa bado kundi hilo linatekeleza mauaji na utekaji nyara kwa wananchi katika ukanda  huo na hivyo

(SAUTI CHERIF)

‘‘Boko Haram wamemedhoofishwa kijeshi lakini haijashindwa kabisa na inasalia tishio kubwa na wana uwezo wa kujipanga tena kupitia msaada wa mitandao iliyoanzishwa katika ukanda wa Sahel.’’

Kikao hicho kadhalika kimejadili hali ya usalama nchini  Somalia na hali ya kibinadmau  kufautia mgogoro unaoendelea  nchini Syria.