Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya kimataifa ya kukabiliana na homa ya ini, WHO yataka nchi zichukue hatua

Siku ya kimataifa ya kukabiliana na homa ya ini, WHO yataka nchi zichukue hatua

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kupambana na ugonjwa wa homa ya ini au Hepatitis, Shirika la Afya Duniani(WHO) linataka nchi zichukue hatua za dharura katika kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo na kuhakikisha kuwa watu ambao wameathiriwa wanapatiwa tiba. Taarifa kamili na Amina Hassan.

(TAARIFA YA AMINA)

Msisitizo kwa mwaka huu ni aina za Hepatitis B na C ambazo kwa mujibu wa WHO husababisha takribani asilimia 80 ya vifo vyote vya saratani ya ini na hivyo kuuwa watu milioni 1.4 kwa mwaka.

Stefan Wiktor ni kiongozi wa timu ya mpango wa WHO katika kukabiliana na Hepatitis na anasema kumekuwa na mafanikio anuai katika upatikanaji wa dawa za kutibu Hepatitis B ambazo zaweza kudhoofisha virusi na kusaidia kukabili uharibifu wa ini unaoweza kusababishwa na virusi vya Hepatitis B. Kuhusu Hepatitis C anasema.

(SAUTI STEFAN)

”Habari ni njema zaidi kwa Hepatitis C, sasa tuandawa ambazo waweza kutumia kwa majuma 12 na kila mtu aweza kutibiwa. Hii inamaanisha kuwa virusi vinaondoka mwilini na mgonjwa ana nafasi ndogo ya kufa kutokaan na kansa ya ini.”

WHO imesema nchi nyingi barani Afrika na Asia maambukizi mengi ya Hepatitis B ni kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na kushauri utolewaji wa chanjo hatua ambayo imetekelezwa Tanzania kama anavyosema Daktari Janet Mgamba ambaye ni Mkurugenzi msaidizi wa kitengo cha kudhibiti magonjwa ya milipuko nchini humo.

(SAUTI DK JANETH)