Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya kimataifa ya kupinga matumizi ya madawa ya kulevya

Siku ya kimataifa ya kupinga matumizi ya madawa ya kulevya

Juhudi za kukabiliana na madawa ya kulevya ni lazima ziambatane na kazi zetu za kuchagiza fursa kupitia maendeleo sawa na endelevu. Ni lazima tuendelea kujaribu kuwafanya wanyonge na wadhaifu wawe na nguvu. Huo ni ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon wa siku ya kupinga matumizi ya madawa ya kulevya inayoadhimishwa Juni 26 kila mwaka.

Siku hii imekuwa ikiadhimishwa tangu kupitishwa na  Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mnamo Disemba 1987 kama sehemu ya juhudi za ulimwengu kuchagiza vitendo na ushirikiano ili kushinda vita dhidi ya matumizi ya madawa ya kulevya.

Uamuzi huu ulifikiwa baada ya kuonekana pengo licha ya juhudi za jamii ya kimataifa, kwamba matumizi ya madawa ya kulevya yanaathiri afya ya umma, usalama wa binadamu hususan vijana aidha yanahatarisha usalama wa kisiasa na maendeleo endelevu. Licha ya ugunduzi huo mataifa kote ulimwenguni yanaendelea kuukokota mzigo huu ambao unazidi kuwa mzito kila uchao.

Je hali ikoje nchini Kenya huko barani Afrika? Salim Chiro akiwa Pwani ya Kenya anavinjari kutupatia hali halisi ungana naye katika makala hii.