Umoja wa Mataifa pamoja na mashirika ya kibinadamu wako katika kampeni madhubuti wakipigia chepuo agenda ya malengo ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030. Kapeni hiyo inayozijumuisha serikali mbalimbali duniani, ni moja ya njia sahihi ya kuleta usawa na maendeleo kwa nchi masikini kwa mfano upigaji vita uharibifu wa mazingira, kupigania usawa kijinsia, afya bora na ajira zikiwa ni baadhi tu ya malengo andelevu 17 za Umoja wa Mataifa. Dkt. Maro, anazungumzia umuhimu wa malengo ya maendeleo endelevu kwa jamii ya watu wa kipato cha chini hususani huko Afrika ambako watu wengi ni masikini wanaohitaji elimu ya kutosha kuhusu SGDs.