Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umri katika uongozi unakwaza vijana kwenye demokrasia: Hamad Rashid Mohamed

Mh. Hamad Rashid Mohamed katika kikao cha mkutano wa 131 wa IPU. (Picha©IPU/Pierre Albouy)

Umri katika uongozi unakwaza vijana kwenye demokrasia: Hamad Rashid Mohamed

Umoja wa mabunge duniani umekuwa na mkutano wake mkuu wa 131 huko Geneva Uswisi kuanzia tarehe 12 mwezi huu wa Oktoba. Ajenda za mkutano huo ni pamoja na demokrasia na haki za binadamu na dhima ya jamii ya mabunge katika kuchagiza harakati dhidi ya Ebola.

Miongoni wa washiriki ni Hamad Rashid Mohamed, mbunge kutoka Tanzania ambaye katika mahojiano maalum na Assumpta Massoi wa idhaa hii ya Kiswahili ya Radio ya Umoja wa Mataifa ametanabaisha kwa kina muktadha wa kikao hicho.

Kwanza anaanza kuelezea nafasi ya bunge katika kuhabarisha wananchi wanaowaongoza.