Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Harakati za kumkomboa mwanamke

Harakati za kumkomboa mwanamke

Mkutano wa 59 wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW59 unaendelea kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kukiwa na matukio mbali mbali yanayotathimini nafasi ya mwanamke duniani katika nyanja mbalimbali ikiwamo kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Mkutano huu hufanyika kila mwaka, lakini wa mwaka huu ni wa muhimu zaidi kwa kuwa unatathmini miaka 20 baada ya baada ya mkutano wa nne wa kimataifa wa wanawake wa Beijing China ulioweka historia kwa kuweka bayana makubaliano ya msingi kuhusu mustakhbali wa wanawake hususan usawa wa kijinsia. Je nini kinajiri? Basi ungana na Assumpta Massoi katika makala ifuatayo.