Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hospitali ziendelee kufanya kazi wakati wa majanga ili kuokoa maisha:WHO

Hospitali ziendelee kufanya kazi wakati wa majanga ili kuokoa maisha:WHO

Shirika la afya duniani WHO limesema kuziacha hospitali ziendelee kufanya kazi wakati wa majanga ya asili na mlipuko wa magonjwa ni muhimu sana katika kuokoa maisha ya watu.

WHO inasema mkakati huo ambao inauita “mpango salama wa hospitali” tayari umesharidhiwa nan chi 70, na shirika hilo litauwasilisha kwenye mkutano wa tatu wa kimataifa wa kupunguza majanga unaoanza Jumamosi mjini Sendai Japan.

Kwenye mkutano huo Dr. Rick Brennan wa WHO atazitaka nchi kuyaweka masuala ya huduma za afya katika kipaumbele cha sera za dharura.