Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dunia imekutana Japan afiki jinsi ya kukabiliana na hatari ya majanga:

Dunia imekutana Japan afiki jinsi ya kukabiliana na hatari ya majanga:

Wadau mbalimbali kutoka kila penmbe ya dunia wanakutana Japan mwisho wa wiki kwa ajili ya mkutano wa tatu wa kimataifa katika miaka 21 , kuafikiana mtazamo mpya kwa kukabili hatari ya majanga utakaopunguza idadi ya vifo na hasara za kiuchumi. Flora Nducha na taarifa kamili..

(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)

Tangu mkutano wa mwisho wa aina hiyo uliofanyika kobe Japan Januari 2005, takribani watu 700,000 wameaga dunia , huku wengine bilioni 1.7 wameathirika na majanga makubwa yaliyoikumba dunia ikiwa ni pamoja na hasara ya kiuchumi ya dola trilioni 1.4. Bwana Nathan Kigotho ni mkurugenzi wa taifa wa kituo cha operesheni za majanga Kenya anaelezea matumaini yake kwenye mkutano huo..

(SAUTI YA NATHAN KIGOTHO)

Mkutano huu utaanza rasmi siku ya Jumamosi ukihudhuriwa na wakuu wa nchi na serikali, jumuiya za kijamii, mashirika ya kimataifa, pia Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban ki-moon na wadau wengine. Mkutano wa kwanza wa aina hii ulifanyika Yokohama Japan mwaka 1994.