Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

Katika vita dhidi ya virusi vya corona, COVID-19, kitu kikubwa tunaambiwa tuzingatie usafi: Wananchi Geita

Serikali kote duniani zimeendelea kuja na mbinu za kila namna ili kupambana na janga la virusi vya corona, COVID-19.

Sauti -
3'53"

Jinsi ya kuzungumza na watoto kuhusu ugonjwa wa virusi vya Corona

Ni rahisi sana kuhisi kuzidiwa uwezo na kila kitu pindi unaposikia kuhusu ugonjwa wa virusi vya Corona, COVID-19. Ni wazi kuwa watoto wanapata shaka na shuku hasa wanapoona taarifa kwenye runinga au kusikia kutoka kwa watu. Je utazungumza nao vipi? Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limekupatia vidokezo vifuatavyo ili uweze kuibua mjadala na watoto na kuzungumza nao.

COVID-19: Mradi wa UN-Habitat wafanikisha unawaji mikono Mathare, Kenya

Shirika la makazi la Umoja wa Mataifa, UN-Habitat kwa kushirikiana na kituo cha mazingira cha vijana eneo la Mathare jijini Nairobi, Kenya, au  Mathare Environmental One Stop Youth Centre wameungana kwa ajili ya kutoa huduma ya maji safi ya kunawa mikono kwa wakazi 50,000 wa kijiji cha Mlango Kub

Sauti -
1'26"

UN yazindua ombi la dola bilioni 2 kusadia nchi maskini kukabili virusi vya Corona

Umoja wa Mataifa leo umezindua ombi la dola bilioni 2 ili kusaidia harakati za kukabiliana na ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19 katika nchi maskini zaidi duniani.

Mradi wa pamoja wa UN-Habitat ni msaada kwa wakazi wa mtaa wa Mathare, Kenya

Nchini Kenya hatua zaidi zimechukuliwa kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa virusi vya Corona,  COVID-19, wakati wakati huu ambapo tayari serikali imethibitisha kuwepo kwa wagonjwa 28 wa ugonjwa huo.

COVID-19: Uganda yapiga marufuku wakimbizi kuingia nchini humo

Serikali ya Uganda imesema kutokana na kuenea kwa ugonjwa wa virusi vya Corona, COVID-19,  na idadi ya wagonjwa kufikia 14, wakimbizi hivi sasa hawataingia nchini humo huku ikizuia hata huduma za kudhibiti kuenea kwa virusi hivyo zilizokuwa zikitolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR kwenye vituo vya mapokezi ya wakimbizi.

Magereza na rumande zipunguze mirundikano kuepusha kusambaa COVID-19

Ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19 umeanza kusambaa kwenye magereza, vituo vya ushikiliaji wahamiaji wasio na nyaraka na hivyo serikali lazima zichukue hatua kulinda afya za wanaoshikiliwa kwenye maeneo hayo, amesema Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet.

Yemen sitisheni uhasama mjikite na COVID-19:Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito kwa pande kinzani katika mzozo wa Yemen kusitisha uhasama mara moja na kujikita katika majadiliano ya suluhu ya kisiasa huku wakifanya kila wawezalo kukabiliana na virusi vya Corona, COVID-19.

Tufungue bandari zetu ili shehena za dawa na vifaa viweze kusaidia kukabili COVID-19 – UNCTAD

Wakati nchi duniani zinaendelea kupambana na mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya Corona, COVID-19, Umoja wa Mataifa umesema sekta ya usafirishaji majini ina dhima muhimu katika hatua dhidi ya janga hilo.