COVID-19: Uganda yapiga marufuku wakimbizi kuingia nchini humo

25 Machi 2020

Serikali ya Uganda imesema kutokana na kuenea kwa ugonjwa wa virusi vya Corona, COVID-19,  na idadi ya wagonjwa kufikia 14, wakimbizi hivi sasa hawataingia nchini humo huku ikizuia hata huduma za kudhibiti kuenea kwa virusi hivyo zilizokuwa zikitolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR kwenye vituo vya mapokezi ya wakimbizi.

Taarifa iliotolewa leo kuhusu msimamo wa serikali kwa wakimbizi wanaopitia migogoro isiojali mlipuko wa COVID-19 duniani, Musa Ecweru naibu waziri wa wakimbizi na kushughulikia majanga ametangaza rasmi kuwa kamwe kamwe wasakahifadhi hawataruhusiwa tena kukanyaga kwenye ardhi ya Uganda.

Amesema hayo saa chache baada ya kuthibitishwa kwa wagonjwa watano zaidi wa COVID-19 kando na tisa waliothibitishwa kwanzia usiku w aJumamosi wiki iliopita.

Hivyo Bwana Ecweru amesema hawawezi tena kuvumilia wakimbizi zaidi kuingia au kukaa nchini Uganda na kwa kutekeleza azimio hilo, wameanza kufunga mapokezi yote ya wakimbizi mpakani na mpakani na kisha kupunguza idadi ya waliokuwa tayari kwenye mapokezi ya wakimbizi makambini.

Akiongea akiwa mkali bwana Ecweru amesema si kw akuchukia wakimbizi lakini ni kwa kuhakikisha usalama wa Waganda na majirani zake.

Umauzi huo pia umetangazwa rasmi wakati ambapo wakimbizi 20 kutoka Jmahuri ya Kidemokrasia ya Kongo, (DRC) wameweka chini ya karantini ya siku 14 kuchunguzwa hali yao ya virusi vya COVID-19 wakiwa kwenye ufukwe wa Ziwa Albert wilayani Kagadi

Askari mmoja wa mpakani aliyetuhumiwa kuwatorosha kuingia nchini baada ya mpaka kufungwa amekamatwa na polisi.

Duniya Aslam Kahan Msemaji wa UNHCR, Uganda amesema kufuatia uamuzi huo, wameanza kuhamisha kwa dharura wasakahifadhi waliokuwa kwenye mapokezi ya wakimbizi kadi makambini.

Hata hivyo amesema msimamo wa UNHCR ni kuyaomba mataifa kuhakikisha wanatii haki za wakimbizi na makundi mengine yaliohatarini kwa kupunguz avikwazo mipakani na kuzingatia uhuru wa kutembea.

Wagonjwa wapya watano waliothibitishwa leo na Mkurugenzi Mkuu wa Huduma za Afya Henry Mwebesa ni raia wa Uganda watatu akiwemo mtoto mchanga mwneye umri wa miezi minane na Wachina wawili walioingia nchini wiki iliopita.

 

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter

Fuatilia Habari: Habari zilizopita za Mada Hii

Uganda sasa ina wagonjwa 8 wa COVID-19, masoko yote yafungwa

Nchini Uganda serikali imeimarisha juhudi za kudhibiti virusi vya Corona COVID-19 baada ya kuthibitishwa kwa wagonjwa wapya wanane katika nchi hiyo na kuwaacha wananchi wakiwa katika hali ya taharuki. Miongoni mwa hatua mpya zilizochukuliwa sasa ni uamuzi wa kufunga masoko ambayo yalikuwa yameaachwa  wazi na kusababisha bei za bidhaa muhimu kupanda.

Uganda yafunga mipaka yake kwa abiria juu ya COVID-19

Serikali ya Uganda imeamua kufunga mipaka yake yote kwa abiria na kutangaza kuwa ni vyombo vyenye shehena za mizigo pekee ndio vitakavyovuka mipaka na kuingia nchini humo kufuatia kuthibitishwa kwa mgonjwa wa kwanza wa Corona au  COVID-19 nchini humo mwishoni mwa wiki.