UNDP yashindanisha vijana kusaka majawabu kwa tabianchi , washindi kupata kitita cha fedha
Vijana wameelezwa kuwa na umuhimu mkubwa katika kusongesha mbele moja ya ajenda kubwa za 2030 za Umoja wa Mataifa ambayo ni kukabiliana na janga la mabadiliko ya tabianchi. Na katika kutambua mchango wao Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP, limekuja na mbinu mbalimbali za kuwashirikisha vijana ili wasiachwe nyuma katika suala hilo na mengine kama ya kuleta amani na usalama. Olle Mjengwa anayefanyakazi ya UNDP ofisi ya Roma Italia amezungumza na UN News kandoni mwa Jukwaa la vijana la Baraza la Kiuchumi na Kijamii ECOSOC lililokunja jamvi mwishoni mwa wiki ili kufafanua kuhusu ushirikishwaji huo wa vijana katika UNDP