Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNDP yashindanisha vijana kusaka majawabu kwa tabianchi , washindi kupata kitita cha fedha

Olle Mjengwa mshiriki wa Jukwaa la Vijana 2030, la Baraza la Kiuchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa, ECOSOC, akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa kandoni mwa mkutano huo uliofanyika kwa siku tatu, New York ,Marekani.
UN/Assumpta Massoi
Olle Mjengwa mshiriki wa Jukwaa la Vijana 2030, la Baraza la Kiuchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa, ECOSOC, akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa kandoni mwa mkutano huo uliofanyika kwa siku tatu, New York ,Marekani.

UNDP yashindanisha vijana kusaka majawabu kwa tabianchi , washindi kupata kitita cha fedha

Tabianchi na mazingira

Vijana wameelezwa kuwa na umuhimu mkubwa katika kusongesha mbele moja ya ajenda kubwa za 2030 za Umoja wa Mataifa ambayo ni kukabiliana na janga la mabadiliko ya tabianchi. Na katika kutambua mchango wao Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP, limekuja na mbinu mbalimbali za kuwashirikisha vijana ili wasiachwe nyuma katika suala hilo na mengine kama ya kuleta amani na usalama. Olle Mjengwa anayefanyakazi ya UNDP ofisi ya Roma Italia amezungumza na UN News kandoni mwa Jukwaa la vijana la Baraza la Kiuchumi na Kijamii ECOSOC lililokunja jamvi mwishoni mwa wiki ili kufafanua kuhusu ushirikishwaji huo wa vijana katika UNDP


 

Olle amesema binafsi anafanya kazi ya ya kushirikisha vijana kwani UNDP ina miradi mbalimbali ambayo iko katika kanda ya Afrika, hususan Kusini mwa Afrika, Mashariki ya Kati na kanda ya Asia.

Amesema kikubwa wanachofanya ni “Kujaribu kufadhili miradi inayofanywa na vijana na hasa katikia sekta ya mazingira, mabadiliko ya tabianchi lakini pia nishati.”

Je ni miradi hiyo ni ya aina gani ?

Olle amesema miradi hiyo mfano ni ile ambayo inatumia ubunifu katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi.

Akitoa mfano amesema mathalani “nchini Uganda kuna mama mmoja ametengeneza Apu ya kuwaunganisha wakulima na wamiliki wa ardhi ili kuongeza uzalishaji wa mazao nchini humo.”

Kuhusi jinsi wanavyoweza kuwapata vijao hao kushiriki katika mitadi hiyo Olle amesema “tuna shinadno la kusaka majawabu dhidi ya mabadiliko ya tabianchi. Na lengo kuu ni kupata washindi 50 ambao tutawafadhili kwa kuwapa dola elfu 30 ili kuendesha miradi yao katika sekta ya mazingira, mabadiliko ya tabianchi na nishati”

Jinsi ya kushiriki shindano hilo

Ili vijana waweze kuushiriki katika shindano hilo Olle amesema “kwanza ni lazima warambaze kwenye wavuti wetu wa youth for climate , pia wanaweza kutufuatili kwenye mitandao ytu ya kijamii ya youth for climate au kwenye ukurasa wa UNDP Rome center ambako wanaweza kupata raarifa zote za kuweza kuomba kushiriki katika shindano letu. Na shindano hili liko wazi hadi tarehe 26 Mei.”

Olle amewachagiza zaidi vijana kutoka Afrika Mashariki kuchangamkia fursa hiyo adhimu akisistiza kuwa “cha muhimu ni kwamba kuhakikisha mradi wako unatumia ubunifu dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, pia tunapenda sana miradi ambayo inasaidi katika kuchagiza usawa wa kijinsia katika jamii na tunataka kuwasaidia vijana katika mchakato wa kuomba ufadhili.”

Mbali ya hayo amesema katika wavuti wao kuna fursa nyingine nyingi ikiwemo vijana kupata fursa ya ushauri, wanaweza kuona semina za jinsi ya kuandaa maombi mazuri ya ushiriki hivyo amewataka vijana wajitokeze na wasiogope wote wenye mawazo na fikra mpya ili kukumbatia fursa hizo.

Kwa nini mchango wa vijana ni muhimu katika vita dhidi ya tabianchi?

Olle ambaye yeye mwenyewe ni kijana anasema katika  UNDP wanaamini kwamba “vijana ndio wana mawazo mapya, vijana wana ubunifu kwani tayari tuna mifano mingi ya miradi muhimu ambayo inakabilina na athari za mabadiliko ya tabianchi.”

Kwa hiyo amesem ni “muhimu kwetu kuwapa vijana nafasi , kuwapa vijana fursa na kuwapa vijana ufadhili katika lengo lao la kutusaidia kwenye vita dhidi ya janga hili la mabadiliko ya tabianchi”

Akiwageukia vijana akiwemi yeye mwenyewe Olle amekumbusha kwamba “Mhango wetu ni muhimu sana, tunao uwezo, tusiogope na tukumbatie fursa zilizopo.”

Kwani amesema kama vijana mara nyingi wanakabiliana na vikwazo ambavyo ni vingi lakini zinazpojitokeza fursa kama mradi wa youth for climate unaowapa vijana ufadhili basi wachangamkie fursa hizo.  

Amesema kwa kufanya hivyo itakuwa fursa nzuri pia ya kuonyesha kwamba vijana tunao uwezo wa kupambana na mabadiliko ya tabianchi na tuna mawazo mapya na ubunifu wa kufanya mabadiliko makubwa katika kila sekta ya maendeleo lakini hususan katika vita dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.”

Amani, usalama na vijana

Olle Mjengwa (kushoto) mshiriki wa Jukwaa la Vijana 2030, la Baraza la Kiuchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa, ECOSOC, akizungumza na Flora Nducha wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa kandoni mwa mkutano huo uliofanyika kwa siku tatu, New York ,Mar…
UN/Assumpta Massoi
Olle Mjengwa (kushoto) mshiriki wa Jukwaa la Vijana 2030, la Baraza la Kiuchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa, ECOSOC, akizungumza na Flora Nducha wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa kandoni mwa mkutano huo uliofanyika kwa siku tatu, New York ,Marekani.

Olle amesema mbali ya kujikita na masuala ya mabadiliko ya tabianchi UNDP pia inawashirikisha vijana katika masuala ya amani na usalama.

Amesema hii ni kutokana na ukweli kwamba Afrika na sehemu nyingine nyingi duniani migogoro mingi inatokea kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi na kwamba “Vijana wana nafasi muhimu katika jamii kupambana na mabadiliko ya tabianchi lakini pia kuleta amani katika jamii zao kwani tunaamini kabisa kwamba vijana wako msitari wa mbele kuleta amani.”

Ameongeza kuwa wanachojaribu kufanya ni “kutumia mtazamo wa pamoja unaojumuisha sekta ya mabadiliko ya tabianchi, mazingira, Amani na vijana kwa sababu tunaamini kwamba bila vijana hakuna amani.”

Amesisitiza kwamba ni muhimu kutambua kwamba mabadiliko ya tabianchi yanaathiri na yanasababisha migogoro kwa hiyo “tunajaribu kufanyakazi katika sekta hiyo na pian a mashirika mengine ndani na nje ya Umoja wa Mataifa kufanikisha hilo.”