Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

DRC: Mapigano na mizozo vyanyima wananchi manufaa ya utajiri wa nchi yao- Türk

Familia moja iliyokimbia makazi yao sasa inaishi katika kambi ya muda huko Plain Savo, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. (Maktaba)
© UNHCR/Hélène Caux
Familia moja iliyokimbia makazi yao sasa inaishi katika kambi ya muda huko Plain Savo, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. (Maktaba)

DRC: Mapigano na mizozo vyanyima wananchi manufaa ya utajiri wa nchi yao- Türk

Haki za binadamu

Kaminshna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu Volker Türk ambaye yuko katika ziara rasmi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC amestaajabu ni kwa vipi utajiri wa maliasili uliosheheni kwenye taifa hilo umeleta manufaa kidogo kwa wananchi wako kutokana na ghasia na mapigano. 

Video ya Umoja wa Mataifa inaanzia Kinshasa mji mkuu wa DRC ambako Bwana Türk na aafisa mmoja wa Umoja wa Mataifa wanatazama ramani ya taifa hilo lililoko Maziwa Makuu na kisha anasema ni moja ya nchi tajiri zaidi duniani, lakini tunaona ni kwa vipi utajiri huu kwa bahati mbayá hauko kunufaisha wananchi kwa sababu ya mapigano.

Na kisha anaelezea mipango ya ziara yake ya kutathmini hali ya haki za binadamu akisema kwanza ni kukutana na watu waliofurushwa makwao kutokana na ghasia na vile vile kuonana na mamlaka husika na mashirika ya kiraia.

Baada ya hapo safari inaanza akiambatana na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo, Bintou Keita, mwelekeo ni Mashariki mwa nchi jimboni Ituri. Taswira ya angani kutoka ndege hii ya Umoja wa Mataifa na kisha wanawasili. Mapokezi hapa Bunia, kutoka kwa wenyeji wao.

Moja kwa moja msafara wao wa magari unafika kwenye kambi ya wakimbizi nje kidogo ya mji wa Bunia na wanaingia ndani ambako wanawake, wanaume na watoto, wazee na vijana, nyuso zao zinaonesha matuamini kwani wahenga walinena mgeni njoo mwenyeji apone.

Mkalimani akamweleza Turk kuwa wanachosema maeneo yao yametawaliwa na waasi na hawawezi kurejea makwao.

Na ndipo Kamishna huyu Mkuu wa Haki za Binadamu baada ya kuwasikiliza wakimbizi na kuzungumza nao akatoka nje na kusema, “Nimekutana na kundi la watu ambao wamefurushwa makwao kutokana na mauaji ya kikatili na ya kutisha yaliyotekelezwa kwenye makazi yao. Na wamekuweko hapa kwa miaka minne sasa. Tamanio lao kubwa kabisa ni kuweza kurejea makwao.”

Kwa sasa kuna takribani watu milioni 1.8 waliofurushwa makwao jimboni Ituri kati ya wakimbizi wote wa ndani milioni 7.2 nchini kote DRC.

Bwana Turk amerejea Kinshasa ambapo kesho Alhamisi atakuwa na mazungumzo na Rais Félix Tshisekedi na maafisa wengine wa serikali, Umoja wa Mataifa, wanadiplomasia na vyama vya siasa pamoja na watetezi wa haki za binadamu na kisha atazungumza na waandishi wa habari.

Mama huyu ambaye jina lake limehifadhiwa kwa sababu za kiusalama ni wa eneo la Afar, mashariki mwa Ethiopia ambako pia kumeathiriwa na mafuriko anapaza sauti akisema, “Ninataka kulea na kusomesha watoto wangu vizuri. Nawatakia watoto wangu mema.”

Umoja wa Mataifa na wadau wa kibinadamu wanaunga mkono mwitikio wa kitaifa wa kuongeza msaada wa kuokoa maisha kwa watu milioni 15.5, na msaada wa chakula kwa watu milioni 10.4 nchini humo Ethiopia. Kwa mwaka mzima, ili mpango huo ufanikiwe unahitaji dola za Marekani bilioni 3.24.