Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Naumia moyo kuona waislam wengi hawasherehekei Eid El Fitr kwa amani: Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres
UN Photo/Eskinder Debebe
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres

Naumia moyo kuona waislam wengi hawasherehekei Eid El Fitr kwa amani: Guterres

Masuala ya UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema Eid Al Fitr ni wakati ambao kila mwaka hupenda kutoa salamu zake kwa waislam wote duniani akiwatakia kila la heri na fanaka ya kusherehekea baada ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani. 

 

Lakini kupitia ujumbe wake mfupi wa video mahsusi kwa siku hii Guterres amesema mwaka huu hali ni tofauti ingawa anawatakia jumuiya yote ya Waislam wote kote duniani Eid Mubarak.

 Ameongeza kuwa pamoja na salam hizo za Eid ana masikitiko makubwa akisema “moyo wangu umejawa na machungu makubwa kwamba, huko Gaza, Sudan, na maeneo mengine mengi kwa sababu ya migogoro na njaa, waislamu wengi hawataweza kusherehekea Eid ipasavyo.”

Eid Al Fitr ni moja ya sikuu kubwa zinazoadhimishwa na waislam kila mwaka mwezi ukiandama baada ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Sikukuu hii inaadhimishwa huku mizozo ikiwa imeshamiri kwenye maeneo kuanzisha huko Mashariki ya Kati kwenye Ukanda wa Gaza, Ukraine, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Syria, Sudan Kusini, Sudan na Myanmar ambako mamia ya maelfu ya wakimbizi wa kabila la Rohingya bado wanaishi kwenye kambi huko Cox's Bazar nchini Bangladesh.