Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Kwenye miteremko ya Nepal, vijiji vinajitayarisha kukabiliana na mvua za Monsoon zinazozidi kuwa mbaya.
UNEP/Artan Jama

UNEP yatoa mbinu za ujenzi unaozingatia hali ya hewa

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira duniani, UNEP kwakushirikiana na chuo kikuu cha Yale kitivo cha mifumo ya ikolojia na usanifu Yale CEA wamezindua ripoti inayoangazia ujenzi unaozingatia hali ya hewa na kutoa mapendekezo matatu ambayo yanatoa suluhu za kuondoa kaboni katika majengo na kupunguza taka zinazozalisha wakati wa ujenzi. 

Mafuriko yamekumba maeneo ya kaskazini mashariki mwa Libya.
© National Meteorological Centre, Libya

Takriban watu 3, 000 wamekufa na 10,000 hawajulikani waliko kufuatia mafuriko Libya:WMO/WHO/IOM/IFRC

Mafuriko makubwa yaliyoikumba Libya tarehe 10 September yamesababisha maafa ikiwemo vifo vya takriban watu 3,000 na wengine zaidi ya 10,000 kutojulikana waliko Mashariki mwa nchi hiyo  kwa mujibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na shirikisho la kimataifa la chama cha msalaba mwekundu IFRC na mwezi mwekundu.

Bango lililoko nje ya Ofisi ya Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja mkabala na jumba la KICC ilikofanyika mikutano ya wiki ya tabianchi.
UN News/Thelma Mwadzaya

Elimisha zaidi umma kuhusu sayansi ya tabianchi ili raia wapate ufahamu - Wanamazingira Afrika

Wanaharakati na watetezi wa mazingira wametoa wito kwa wadau kujikita zaidi katika juhudi za kuuelimisha umma kuhusu sayansi ya tabia nchi ili raia wapate ufahamu. Wanamazingira hao wametoa tathmini hiyo jijini Nairobi nchini Kenya wakizungumza na mwandishi wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa nchini humo Thelma Mwadzaya.

Sikuzani Abdallah (kushoto) ni mkazi wa kata ya Mbagala yenye wakazi wengi Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.
UNCDF/Tanzania

Tanzania katika mwelekeo wa kutumia nishati jadidifu majumbani

Nchini Tanzania kuna kaya nyingi ambazo zinatumia mkaa, kuni na mafuta ya taa kama tegemeo kuu la mapishi ya nyumbani, nishati ambazo si rafiki sio tu kwa mazingira bali pia afya ya mamilioni ya binadamu. Lakini sasa kuna mabadiliko,wakati huu ambapo Umoja wa Mataifa unapigia chepuo nishati jadidifu na salama; wakati huu ambapo pia wakuu wa nchi watakutana jijini New York, Marekani kutathmini hatua zipi zimechukuliwa kubadili mwelekeo wa mabadiliko ya tabianchi.  

Tetemeko la ardhi lililokuwa na kitovu katika milima limesababisha uharibifu katika jiji la kihistoria la Marrakech, Morocco.
UNESCO/Eric Falt

Waliopoteza maisha kwenye tetemeko Morocco wafika 2500, UN iko tayari kusaidia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameelezea mshikamano wake kwa serikali na watu wa Morocco katika kipindi hiki kigumu baada ya tetemeko la ardhi ambako kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura OCHA takwimu zilizotolewa n amalaka ya Morocco zinasema idadi ya waliopoteza maisha kufikia leo ni 2500 na waliojeruhiwa ni 2500.

 

Wakazi wa makazi duni ya Mzambarauni Pwani ya Kenya (Agosti 2018)
© UN-Habitat/Kirsten Milhahn

Haki ya makazi bado ni ndoto kwa wengi duniani- Türk

Mkutano wa 54 wa Baraza la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu umeanza hii leo huko Geneva, Uswisi ambapo Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Volker Türk pamoja na mambo mengine amesisitiza suala la makazi kama moja ya haki za msingi za binadamu na haki inayopigiwa chepuo pia kwenye malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.

Sauti
2'15"