Makaburi ya wafalme wa Buganda yaondolewa kwenye orodha ya UNESCO, kulikoni?
Baada ya kunusurika kwa moto na hatimaye kuwekwa kwenye orodha ya maeneo ya urithi wa dunia yaliyo hatarini kuharibika, makaburi ya wafalme wa Buganda huko Kasubi nchini Uganda sasa yako salama na yameondolewa kwenye orodha hiyo baada ya ukarabati uliofanywa na Uganda kwa usaidizi wa Umoja wa Mataifa na wadau.