Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Mwezi
NASA

Leo ni siku ya kimataifa ya mwezi

Leo ni siku ya kimataifa ya mwezi ambapo Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilitangaza siku hii ya kimataifa iliyoteuliwa na Umoja wa Mataifa kuadhimishwa kila mwaka tarehe 20 Julai, katika azimio lake nambari 76/76 kuhusu "Ushirikiano wa Kimataifa katika matumizi ya amani ya anga za mbali" mwaka 2021.

Gavana wa Kauti ya Kakamega Fernandes Baraza (Katikati) pamoja na Mbunge wa Likuyani Innocent Mugabe ( wa kwanza kushoti) wakiwa katika mahojiano na Leah Mushi( wa kwanza Kulia) katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
UN News

HLPF: Safari bado ndefu kutimiza SDGs duniani

Jukwaa la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu lijulikanalo kama HLPF linafikia tamati hii leo hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York-Marekani baada ya siku 10 za majadiliano ya nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa juu ya utelekelezaji wa SDGs katika nchi zao, maendeleo na changamoto walizokutana nazo ikiwa ni miaka 15 tangu kuanza utekelezaji wake ambao unatarajiwa kufikia tamati mwaka 2030. 

Sauti
8'15"
Aliyeketi kati ni Gibson Kawago, mmoja wa viongozi vijana wa Umoja wa Mataifa wa kusongesha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs akiwa anafuatilia kikao cha vijana kuhusu kuchagiza SDGs kando ya Jukwaa la ngazi ya juu la kisiasa, HLPF linalofanyika kwenye…
UN/Assumpta Massoi

Vijana wengi wanasoma lakini elimu haiwawezeshi kutatua changamoto za kijamii - Gibson

Hii leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa,  Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu kuhusu vijana amezindua ripoti ya  mwaka huu wa 2023 ya utekelezaji wa Mkakati wa UN kuhusu vijana, ripoti ambayo kwa kiasi kikubwa inaonesha mafanikio yaliyokana na Umoja wa Mataifa kutekeleza ahadi zake kwa vijana, hususan ushirikishaji wa vijana katika kusongesha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs yanayofikia ukomo wake mwaka 2030.

Sauti
2'31"