Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

HLPF ikifunga pazia nusu ya muda wa utumizaji SDGs, dunia inasuasua

Malengo ya Maendeleo Endelevu ni mwongozo wa kufikia mustakabali bora na endelevu kwa wote.
© UNDP
Malengo ya Maendeleo Endelevu ni mwongozo wa kufikia mustakabali bora na endelevu kwa wote.

HLPF ikifunga pazia nusu ya muda wa utumizaji SDGs, dunia inasuasua

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Jukwaa la ngazi ya juu la Umoja wa Mataifa la kisisa kuhusumalengo ya maendeleo endelevu HLPF, limefunga pazia mjini New York Marekani leo tarehe 19 Julai na kuweka msingi kwa ajili ya  mkutano muhimu wa SDG utakaofanyika mwezi Septemba.

Katika siku kumi zilizopita, viongozi wa dunia, watunga sera, na washikadau wakuu walikusanyika ili kutathimini maendeleo, kubadilishana uzoefu, na kujadili mikakati ya kuendeleza maendeleo endelevu.

HLPF inatumika kama jukwaa kuu la ufuatiliaji na mapitio ya utekelezaji wa SDGs, ambayo yalipitishwa na nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa mwaka 2015. 

Malengo haya ni mjumuiko wa malengo 17 ikiwa ni pamoja na kutokomeza umaskini, kukuza usawa wa kijinsia, kuhakikisha upatikanaji wa elimu bora na huduma za afya, na kulinda mazingira.

Likiwa limejikita katika maudhui “Kujikwamua kuliko endelevu na kwenye mnepo dhidi ya janga la COVID-19”, HLPF ya mwaka huu imetambua changamoto ambazo hazijawahi kutokea zinazoletwa na majanga ya afya ulimwenguni.

Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres akizungumza wakati wa kufunga jukwaa la ngazi ya juu la Umoja wa Mataifa HLPF
UN Photo/Loey Felipe
Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres akizungumza wakati wa kufunga jukwaa la ngazi ya juu la Umoja wa Mataifa HLPF

Athari kubwa za COVID-19

Janga la COVID-19 limekuwa na athari kubwa kwa nyanja zote za jamii, na kuzidisha pengo la ukosefu wa usawa lililopo na kuzuia maendeleo kuelekea SDGs. Kongamano hilo lililenga kubainisha suluhu na mikakati ya kujiimarisha vyema katika ulimwengu wa baada ya janga hilo.

Wakikiri kwamba ulimwengu "uko nje ya mstari wa kufikia SDGsifikapo tarehe ya mwisho ya mwaka 2030, maafisa wakuu wa Umoja wa Mataifa, mawaziri na watunga sera pamoja na wawakilishi wa sekta binafsi na makundi makubwa ya umma wamejadili njia za kusukuma mbele utekelezaji wa malengo matano kati ya 17 SDGs.”

Waliweka chini ya tathmini maendeleo yaliyopatikana hadi sasa katika upatikanaji wa maji safi, usafi wa mazingira na nishati kwa wote, na kupitia upya njia za kutumia fursa ya teknolojia mpya, pia wakijadili jukumu muhimu la maendeleo ya mijini.

Lachezara Stoeva, Rais wa Baraza la Kiuchumi na Kijamii  la umoja wa Mataifa ECOSOC, ambaye aliongoza kazi ya jukwaa hilo, amesisitiza umuhimu wa uvumbuzi, teknolojia, na ushirikiano wenye matokeo makubwa.

"Tuko katikati ya kufikia ukomo wa malengo hapo 2030 na bado tuko mbali kutimiza SDGs. Habari mbaya ni kwamba tumepoteza miaka saba. Habari njema ni kwamba, bado tuna miaka saba na ushindi unaweza kufikiwa,” 

Moja ya malengo ambayo Rais wa ECOSOC alikuwa nayo kwa jukwaa hilo ni kuongeza ushiriki wa vijana.

"Bila ya kusema, kushirikisha vijana katika majadiliano sio uungwana, ni jambo la lazima kabisa ikiwa tunataka kutimiza Malengo hayo," Bi. Stoeva amesisitiza.

Lachezara Stoeva,  Rais wa ECOSOC akizungumza wakati wa jukwaa la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu HLPF
UN Photo/Eskinder Debebe
Lachezara Stoeva, Rais wa ECOSOC akizungumza wakati wa jukwaa la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu HLPF

Tathmini za kitaifa

Katika jukwaa hilo la HLPF, washiriki walijihusisha katika mijadala zaidi ya 200 ya ngazi ya juu, midahalo shirikishi, na Tathmini za Hiari za Kitaifa. 

Nchi thelathini na nane zilitoa takwimu kuhusu maendeleo yao kuelekea kufikia SDGs, mojawapo ya vipengele muhimu vya ajenda ya maendeleo. 

Hasa, kwa mara ya kwanza kabisa, Umoja wa Ulaya uliwasilisha mapitio yake.

Mojawapo ya mambo muhimu ya kuchukua kutoka kwa HLPF ilikuwa utambuzi kwamba kufikia SDGs kunahitaji juhudi za pamoja zinazohusisha serikali, mashirika ya kiraia, makampuni ya biashara na watu binafsi.

Ni muhimu kukuza ushirikiano wa wadau mbalimbali na kukusanya rasilimali ili kuharakisha maendeleo kuelekea malengo. 

Sekta binafsi haswa, ina jukumu muhimu la kutekeleza katika kukuza ukuaji wa uchumi endelevu na shirikishi kupitia mazoea ya kuwajibika ya biashara na uwekezaji.

Washiriki walihitimisha kwa kusema “Wakati HLPF inapoisha, ni muhimu kuendeleza kasi iliyojitokeza wiki hii.”

Mambo yaliyowasilishwa wazi katika jukwaa hilo, ni muhimu kwa mafanikio ya mkutano wa SDG mwezi Septemba.

Lachezara Stoeva aliwahimiza washiriki wa HLPF, akihitimisha kikao cha Jukwaa hilo kwa kusema "Kwa pamoja ni lazima tufanye kila tuwezalo ili ujumbe wetu usikike kwenye mkutano huo. Ni fursa muhimu ambayo hatupaswi kuikosa,"