Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Upimaji wa homa ya ini Togo
UN

Tunaishi mara moja na tuna ini moja, tutokomeze Homa ya Ini – Dkt. Tedros wa WHO

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni (WHO) Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus kupitia ujumbe wake kwa Siku ya Kimataifa ya Homa ya Ini inayoadhimishwa kila Julai 28, amesema kwa kuwa wanadamu tunaishi mara moja na tuna ini moja, WHO imejitolea kushirikiana na nchi zote na wadau wote ili kutimiza maono ya pamoja ya kutokomeza virusi vya homa ya ini ifikapo 2030.  

Sauti
1'59"
Wakimbizi kutoka Burkina Faso wakiwasili Togo baada ya kuikimbia nchi yao kutokana na ghasia.
© UNHCR/Fidélia Bohissou

Chondechonde msiwarejeshe kwa nguvu wanaokimbia Burkina Faso hali si shwari: UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR, leo limetoa mwongozo mpya juu ya ulinzi wa watu wanaokimbia Burkina Faso, na wito wa haraka kwa mataifa yote kuacha kuwarudisha kwa nguvu watu wote wanaotoka katika ukanda huo ulioathiriwa zaidi na mgogoro unaoendelea nchini humo na badala yake kuwaruhusu raia wanaokimbia Burkina Faso kuingia katika mipaka yao.

Sauti
2'33"
Koketso Mukubani akisimama nje ya Kituo cha Matibabu cha Sediba Hope huko Tshwane, Afrika Kusini. Anasema wanaotumia dawa za kulevya wanapaswa kujumuishwa kwenye mipango na utekelekezaji wa kinga, tiba na huduma dhidi ya VVU na Homa ya ini C.
© UNODC

Simulizi Yangu: Kuishi na Homa ya Ini aina ya C nchini Afrika Kusini

Koketso Mokubane, mwanaume huyu raia wa Afrika Kusini alibainika kuwa na Homa ya Ini C. Amesimama nje ya kituo cha matibabu cha Sediba Hope kwenye kitongoji cha Tshwane. Koketso anafanya kazi ya kwenye ofisi ya Mtandao wa Watu wanaotumia dawa za kulevya nchini Afrika Kusini. Hili ni shirika lisilo la kiserikali linalopata msaada kupitia ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kukabiliana na Dawa na Uhalifu, (UNODC) kwa lengo la kutetea haki za watu wanaotumia dawa za kulevya.

Halijoto imevunja rekodi ya juu zaidi kote ulimwenguni mwaka huu wa 2023.
© Unsplash/Fabian Jones

“Ulimwengu unachemka, viongozi ongozeni”: Guterres

Kufuatia ripoti iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya hewa WMO kwa kushirikiana na lile la Kamisheni ya Muungano wa Ulaya ambayo imethibitisha kuwa mwezi huu wa Julai utavunja rekodi ya dunia ya kuwa na joto kali ulimwenguni kote, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema takwimu hizi mpya ni uthibitisho kuwa ubinadamu umeketi katika kiti cha moto na kwamba lazima hatua zichukuliwe haraka.

Naibu Katibu Mkuu Amina Mohammed akihutubia wakati wa kufunga Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mifumo ya Chakula +2  mjini Rome, Italia.
FAO/Alessandra Benedetti

UNFSS+2 yahitimishwa huko Roma viongozi waeleza mwelekeo

Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mifumo ya Chakula +2 (UNFSS+2) umefikia tamati leo Jumatano katika makao makuu ya  Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) baada ya siku tatu vikao vya ngazi ya juu, mikutano na midahalo iliyowaleta Pamoja mjini Roma, Italia washiriki zaidi ya 2000 kutoka nchi 180, wakiwemo zaidi ya Wakuu 20 wa Nchi na Serikali na Mawaziri 125, ili kuchunguza changamoto na fursa za kubadilisha mifumo ya kilimo cha chakula.