Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Mkunga nchini Kenya akitumia kifaa  cha kuchunguza hali ya ujauzito tumboni mwa mama. Kifaa hiki anaweza kwenda nacho kokote kutoa huduma hiyo hata majumbani.
© UNFPA Kenya

Mwanamke 1 anakufa kila baada ya dakika 2 kutokana na ujauzito- UN

Ni ajabu na kweli kwamba uzoefu unaotakiwa wa matumaini na chanya umegeuka kuwa shubiri na machungu kwa wanawake wajawazito amesema Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO, Dkt. Tedros Ghebreyesus baada ya ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa kufichua hii leo ya kwamba kila baada ya dakika 2 mwanamke mmoja anakufa kutokana na ujauzito au wakati anajifungua mtoto. 

Mkoani Njombe kusini mwa Tanzania, mapishi mbalimbali kutokana na matumizi ya mikunde. Hii inafuatia mafunzo yaliyowezeshwa na FAO na AgriConnect.
FAO Tanzania

Nyama ikiingia mezani, mikunde hunyanyapaliwa- FAO

Jamii ya mikunde! Wengi wanaitambua zaidi kama ni kunde zenyewe, na maharagwe lakini ni zaidi ya hiyo. Kuna choroko, mbaazi, dengu, njegere na kadha wa kadha ambapo kutokana na umuhimu wake sio tu kiuchumi bali pia katika lishe ya binadamu, kurutubisha udongo na pia kuhimili mabadiliko ya tabianchi, ndio maana Umoja wa Mataifa unapigia chepuo.

Sauti
4'55"
Watu wakipita karibu na jengo lililoharibiwa na bomu huko Chernihiv kaskazini mwa Ukrainia.
© UNDP/Oleksandr Ratushniak

Mjadala kuhusu Ukraine: Vita si suluhu; vita ni tatizo 

Mkutano maalumu wa 11 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ulioanza Jumatano hii unaendelea katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani hadi Alhamis hii ya kuamkia tarehe 24 Februari ambayo ni siku unapotimia mwaka mmoja tangu Urusi ilipoivamia Ukraine katika vita inayoendelkea hadi leo. 

Jengo la kihistoria katikati mwa mji wa zamani wa Kharkiv limeharibiwa vibaya kutokana na vita nchini Ukraine.
© UNICEF/U.S. CDC/Christina Pashinka

Uharibifu wa makusudi wa utamaduni wa Ukraine lazima ukome: Wataalam wa haki za binadamu.

Takriban mwaka mmoja baada ya vita kamili kuzuka nchini Ukraine na huku kukiwa na mashambulizi mapya ya makombora yanayolenga mji wa Mashariki wa Kharkiv siku ya Jumatano wataalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wametoa wito wa kukomeshwa mara moja uharibifu wa makusudi wa hazina za kitamaduni za nchi hiyo unaofanywa na vikosi vya Urusi. 

Shule ambayo watoto wa Kipalestina wanahudhuria huko Jerusalem Mashariki.
Reem Arouri

Malengo yetu yako palepale kukomesha machafuko na ukaliaji wa ardhi ya Palestina: Guterres

"Hadhi ya Jerusalem haiwezi kubadilishwa kwa vitendo vya upande mmoja. Malengo yetu yanabaki palepale kukomesha uvamizi huo na kufikia suluhu ya kuwa na serikali mbili ya Israel na Palestina," huu ni msimamo wa Umoja wa Mataifa, ambao Katibu Mkuu wake amesisitiza leo, akionya dhidi ya kuongezeka kwa mvutano na machafuko, na kusisitiza kujitolea kwake kufanya kazi kwa ajili ya haki ya amani. 

Mkulima akimwagilia mboga kwa kutumia maji kutoka bwawa la Guerin-Kouka  nchini Togo
FAO

Nchi za Afrika wekeni mikakati ya usimamizi bora wa matumizi ya maji- FAO

Ni wakati kufikiria upya jinsi ya kutumia maji kwa njia endelevu na yenye uwiano huku ubunifu katika kilimo ukiwa kitovu cha mipango yote,  amesema Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO limesema  Qu Dongyu hii leo wakati akizungumza na viongozi na wataalamu wa Afrika kwenye warsha ya kwanza ya kikanda kuhusu mwelekeo wa matumizi ya maji barani Afrika, warsha inayofanyika nchini Zimbabwe.

Sauti
1'47"
Ndoto ya Thérèse (pichani) ni kuwa Gavana wa jimbo la Tanganyika. Hapa ni katika darasa jipya lililojengwa kwenye shule ya msingi ya Lubile jimboni Tanganyika kwa msaada wa UNICEF na Education Cannot Wait.
© UNICEF/Josue Mulala

UNICEF na ECW yarejesha matumaini kwa watoto waiotumikishwa vitani DRC

Mradi mpya wa shule  nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC uliozinduliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto,  UNICEF na wadau wake kwa ufadhili kutoka mfuko wa Umoja wa Mataifa wa kuchagiza elimu kwenye maeneo ya mizozo, Education Cannot Wait, ECW, au Elimu Haiwezi Kusubiri umewezesha watoto waliokuwa wametumikishwa vitani kuanza kurejea kwenye masomo na hata kutangamana na wenzao kwa amani.  

Sauti
2'45"