Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi za Afrika wekeni mikakati ya usimamizi bora wa matumizi ya maji- FAO

Mkulima akimwagilia mboga kwa kutumia maji kutoka bwawa la Guerin-Kouka  nchini Togo
FAO
Mkulima akimwagilia mboga kwa kutumia maji kutoka bwawa la Guerin-Kouka nchini Togo

Nchi za Afrika wekeni mikakati ya usimamizi bora wa matumizi ya maji- FAO

Tabianchi na mazingira

Ni wakati kufikiria upya jinsi ya kutumia maji kwa njia endelevu na yenye uwiano huku ubunifu katika kilimo ukiwa kitovu cha mipango yote,  amesema Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO limesema  Qu Dongyu hii leo wakati akizungumza na viongozi na wataalamu wa Afrika kwenye warsha ya kwanza ya kikanda kuhusu mwelekeo wa matumizi ya maji barani Afrika, warsha inayofanyika nchini Zimbabwe.

Mkutano huo ni wa siku tatu na leo ikiwa ni ufunguzi ulioleta viongozi wa ngazi ya juu, Bwana Qu amesema Mikakati ya Kitaifa kuhusu mwelekeo wa matumizi yam aji itasaidia kuimarisha mbinu za usimamizi wa maji ambazo ni muhimu katika kutatua changamoto nyingi zinazozingira kwenye matumizi ya maji, na hivyo kusaidia kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu ifikapo mwaka 2030. 

Amesema maji ni moja ya rasilimali adhimu duniani na ni kitovu cha mafanikio ya ajenda 2030 kwa sababu “maij ni chakula, chakula ni maji, chakula ni uhai. Zaidi ya asilimia 95 ya chakula tunachokula kinazalishwa kutoka ardhini, kutoka kwenye udongo na maji. Lakini bado tunakabiliwa na changamoto kubwa za maji: ukame na uhaba wa maji, mafuriko na uchafuzi wa vyanzo vya maji.” 

Ametanabaisha kuwa ni dhahiri janga la tabianchi linaongeza ukali wa ukame na mafuriko ambavyo vyote vina madhara kwenye uzalishaji wa chakula. 

Mkurugenzi Mkuu huyo amesema kilimo kikitumia asilimia 70 ya maji duniani ni lazima sasa kutumia ubunifu kusaka mbinu za matumizi ya maji kwa tija kwa kuwa uzalishaji zaidi unahitaij maji zaidi. 

Majawabu kama vile usimamizi endelevu wa matumizi ya udongo, kuzuia mvurugano wa matumizi ya maji na pia kuhifadhi tabianchi.