Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu milioni 1.5 hawana makazi Uturuki baada ya tetemeko la ardhi: UN

Jengo huko Kahramanmaraş, Türkiye, lililoharibiwa na tetemeko la ardhi.
© UNOCHA/Matteo Minasi
Jengo huko Kahramanmaraş, Türkiye, lililoharibiwa na tetemeko la ardhi.

Watu milioni 1.5 hawana makazi Uturuki baada ya tetemeko la ardhi: UN

Msaada wa Kibinadamu

Wakati idadi ya vifo vilivyotokana na tetemeko la ardhi la Februari 6 nchini Uturuki imefikia watu 41,000, leo wataalam wa maendeleo wa Umoja wa Mataifa wamesema watu milioni 1.5 hawana makazi Kusini mwa nchi hiyo ambako takriban nyumba mpya laki 5 zitahitajika kujengwa.

Louisa Vinton,mwakilishi wa shirika la umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo nchini Uturuki amesema “Hii inafanya tetemeko hilo kwa hakika kuwa kubwa zaidi katika historia ya Ururuki nap engine janga kubwa zaidi la asili kuwahi kuikumba nchi hiyo.”

Matetemeko mengine mawili Zaidi ya ukubwa wa vipimo vya richter 6.4 na 5.8 mtawalia “yamekatili maisha mengine ya watu 6 Jumatatu wiki hii kwenye mpaka wa Uturuki na Syria, kujeruhi watu wengine 294 na majengo mengine kadhaa kuporomoka katika mkoa karibu na Hatay na mengine kwenye pwani ya Mediterranean coast” ameongeza afisa huyo wa UNDP.

Wafanyakazi wa kujitolea wakigawa chakula moto kwa watu waliopoteza makazi yao kutokana na tetemeko la ardhi huko Türkiye.
© UNOCHA/Matteo Minasi
Wafanyakazi wa kujitolea wakigawa chakula moto kwa watu waliopoteza makazi yao kutokana na tetemeko la ardhi huko Türkiye.

Msaada wa kuokoa maisha unaendelea

Kaskazini Magharibi mwa Syria ambako watu milioni 9 wameathirika na tetemeko hilo na wengine 6000 kupoteza Maisha msaada wa kimataifa wa kibinadamu umeendelea kuwasili.

Jumla ya malori 227 yaliyosheheni msaada yamevuka mpaka kutoka Uturuki tangu tarehe 9 Februari  ambapo miongoni mwao malori 195 yalitumia kivuko cha Bab al-Hawa, 22 kivuko cha Bab al-Salam na 10 kivuko cha Al Ra’ee.   

Akizungumza na waandishi wa habari kwa njia ya video kutoka Gaziantep Kusini mwa Uturuki, Dkt. Catherine Smallwood, msimamizi wa matukio ya matetemeko ya ardhi kutoka shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO kanda ya Ulaya  amesema kwamba shirika hilo limesafirisha karibu tani 100 za bidhaa za tiba upande wa pili wa mpaka kutoka Uturuki tangu kutokea kwa janga hilo mbali ya misaada ambao tayari ulikuwa ndani ya Syria.

Msaada uliofikishwa

Vifaa hivi vinajumuisha dawa muhimu, vifaa vya matumizi, dawa za usingizi na ganzi, vifaa vya upasuaji na vifaa vingine vya matibabu kwa ajili ya huduma za ziada kwa watu 40,000 hadi 49,000 wale wanaohitaji msaada wa upasuaji au msaada wa matibabu kwa majeraha mahususi ya tetemeko la ardhi.

Afisa huyo wa WHO ameongeza kuwa vituo 55 vya matibabu vimeharibiwa na kadhaa kusambaratishwa kabisa, lakini kliniki sita zinazohamishika zimetumwa tena katika miji na jamii zinazozunguka Jindires, moja ya maeneo yaliyoathiriwa zaidi kaskazini magharibi mwa Syria.

"Hizi ni kliniki zinazozunguka ambazo hutoa msaada, usaidizi na huduma za matibabu moja kwa moja kwa watu walioathirika" ameeleza Dkt. Smallwood.

Wakaazi walionusurika kwenye tetemeko la ardhi wameachwa katika hali ya baridi kali bila maji ya kunywa, umeme, au mafuta ya kupasha joto nyumba, na wanakabiliwa na hatari ya kuporomoka kwa majengo wanapojaribu kutafuta makazi, imeonya kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya kiuchumi na kijamii kwa Asia Magharibi ESCWA).

Mtoto akiwa baba yake wakisubiri mgao wa msaada kwenye makazi ya muda kusini-mashariki mwa Uturuki
© UNICEF/Özgür Ölçer
Mtoto akiwa baba yake wakisubiri mgao wa msaada kwenye makazi ya muda kusini-mashariki mwa Uturuki

Maendeleo ya misaada ya mstari

Habari zinazowezekana pia ziliibuka kuhusu uwasilishaji wa misaada kutoka Damascus hadi Idlib, ambayo inadhibitiwa kwa kiasi kikubwa na vikosi vya upinzani na ambapo watu milioni 4.1 karibu wanategemea misaada ya kibinadamu, baada ya zaidi ya muongo wa vita nchini Syria.

"Siku ya Jumapili tarehe 19 Februari na Jumatatu tarehe 20, misafara mitatu ya Hilali Nyekundu ya Syria ya misaada ya kibinadamu ilivuka hadi Sheikh Maqsood, eneo linalodhibitiwa na mashirika yasiyo ya kiserikali kaskazini mwa Aleppo. Na kwa hivyo, tunazungumza juu ya mistari hapa," alithibitisha Tommaso Della Longa, msemaji wa Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu (IFRC).

Kufikisha msaada kusikofikika

Habari Njema pia ziliibuka kuhusu uwasilishaji wa misaada kutoka Damascus hadi Idlib, ambayo inadhibitiwa kwa kiasi kikubwa na vikosi vya upinzani na ambako karibu watu milioni 4.1 wanategemea misaada ya kibinadamu, baada ya zaidi ya muongo wa vita nchini Syria.

"Siku ya Jumapili tarehe 19 Februari na Jumatatu tarehe 20, misafara mitatu ya Hilali nyekundu ya Syria iliyosheheni misaada ya kibinadamu ilivuka hadi Sheikh Maqsood, eneo linalodhibitiwa na mashirika yasiyo ya kiserikali kaskazini mwa Aleppo. Na kwa hivyo, tunazungumza juu ya kuvuka mistari hapa" amethibitisha Tommaso Della Longa, msemaji wa shirikisho la kimataifa la vyama vya msalaba mwekundu na Hilali nyekundu (IFRC).

Mbwa wa uokoaji akishiriki katika shughuli ya uokoaji manusura kwenye vifusi kufuatia tetemeko lililokumba Uturuki. Hapa ni katika mji wa Osmaniye.
© UNOCHA/INSARAG
Mbwa wa uokoaji akishiriki katika shughuli ya uokoaji manusura kwenye vifusi kufuatia tetemeko lililokumba Uturuki. Hapa ni katika mji wa Osmaniye.

Kiwango kikubwa cha taka na kifusi

Akiangazia kiwango cha kutisha cha changamoto ya ujenzi mpya inayokuja, Louisa Vinton wa UNDP ameelezea wastani wa tani milioni 116 hadi 210 za kifusi itabidi kuondolewa kwanza.

"Ili kukupa taswira ya kumbukumbu, tetemeko kubwa la mwisho la ardhi nchini Uturuki, mwaka 1999, ambalo pia lilikuwa na idadi kubwa ya waathirika, ingawa ni chini ya nusu ya kile tunachokiona sasa, lilisababisha tani milioni 13 za kifusi. ," amesema.

Katika majanga yaliyopita baada ya matetemeko ya ardhi na milipuko huko Nepal, Haiti, Lebanon, na pia Ukraine, UNDP ina miradi shirikishi ya kuhakikisha kuwa vifusi vinashughulikiwa kwa njia salama za mazingira.

"Taka nyingi zinaweza kutumika tena kwa ajili ya ujenzi na pia zinaweza kutumika kama njia ya kuzalisha mapato kwa muda mfupi," amesema Bi. Vinton.