Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utawala wa Junta Myanmar ni kinyume cha sheria na ni haramu: Thomas Andrews

Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Haki za binadamu nchini Myanmar Thomas Andrews
UN News
Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Haki za binadamu nchini Myanmar Thomas Andrews

Utawala wa Junta Myanmar ni kinyume cha sheria na ni haramu: Thomas Andrews

Haki za binadamu

Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Haki za binadamu nchini Myanmar Thomas Andrews amesema utawala wa kijeshi wa Junta nchini Myanmar ni wa kinyume chas heria na haramu.

Akiwasilisha waraka maalum na kutathimini madai ya utawala wa kisheji kuwa ni serikali ya Myanmar na hatua za kimataifa mjini New York hii leo Bwana Andrews amesema “Katika mkesha wa mwaka wa pili tangu mapinduzi ya kijeshi nchini Myanmar na kuingia mwaka wa tatu utawalla wa kijeshi wa Junta ambao umeunda baraza la taifa la utawala (SAC) bado unasala uhalali wa kuongoza taifa hilo na unaendesha kampeni ya kutafuta kujihalalisha  katika kile kinachoelezewa kuwa ni kufanya uchaguzi ifikapo Agosti 2023.”

Katika mkutano maalum ulioandaliwa na mtaalam huyo na IDEA International na kupewa jina “Kinyume chas heria na haramu” Andrews ameendelea kusema kwamba “Baada ya kushindwa kuunda serikali halali na inayofanyakazi kwa kutumia nguvu Junta inatajibu kubadili mwelekeo kwa manufaa yake kwa kushawishi nchi wanachama kuidhinisha na kukubali uchaguzi wake usio wa halali.” 

Kupuuza madai ya Baraza la Usalama

Pia amesema “Wakati huohuo utawala huo wa kijeshi unaonekana kupuuza madai yaliyotolewa na azimio lililopitishwa hivi karibuni na azimio la Baraza la Usalama namba 2669 (2022) kwa kuendelea kumshikilia kiholela na kumsweka rumande Rais w anchi hiyo na mshauri wa serikali na kampeni yao ya machafuko na vitisho, kupuuza matakwa ya wananchiwaliyoyaeleza kwenye uchaguzi wa mwaka 2020.”

Mtaalam huyo maalum ameainisha jinsi gani SAC isivyo serikali halali ya Myanmar  na jinsi inavyoendelea kukandamiza viongozi waliotangulia na upinzani , ambavyo haiwezi kuendesha uchaguzi, halali ambao unawasilisha matakwa ya wananchi kama msingi pekee halali wa mamlaka ya serikali.

Amesisitiza kuwa “ SAC imeshindwa kukidhi vigezi vikuu viwili ambavyo vinafanya serikali kutambulika kimataifa ambavyo ni mosi udhibiti wa serikali unaofanyakazi na  pili viwango vya uhalali.”

Nchi wanachama zisiisaidie SAC

Kwa vile SAC imekosa uhalali wa kikatiba na kiuchaguzi kuchukua serikali hapo awali, na haina udhibiti mzuri wa nchi, mtaalamu huyo maalumu wa Umoja wa Mataifa  amezitaka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kukataa kutoa msaada wowote kwa SAC, haswa katika jaribio lake la kutaka kufanya uchaguzi ambao hautakidhi hata mahitaji ya chini ili kuzingatiwa kuwa serikali ya kweli.

Amesema hali ya kibinadamu imezidi kuwa mbayá nchini Myanmar tangu utawala wa Junta kushika hatamu kwanu leo mwaka huu 2023 watu milioni 17.6 wanahitaji msaada wa kibinadamu ikilinganisha na watu milioni 1 kabla ya mapinduzi ya kijeshi miaka miwili iliyopita.

Bwana Andrews ametoa mapendekezo ya kusonga mbele na kurejesha serikali ya kidemokrasia na utulivu nchini Myanmar ikiwa ni pamoja na kuiwekea vikwazo serikali ya Junta na kutafuta suluhu ya mgogoro huo kwa njia yenye mshikamano na madhubuti mwaka 2023.

Kuhusu uchaguzi unaotarajiwa 2023

Nayo international IDEA ikiwa na lengo la kuchangia uelewa kwa jumuiya ya kuhusu umuhimu wa uchaguzi, katika mikakati ya jeshi na njia ya shirikisho ya siku zijazo iliyochaguliwa na vikosi vya kidemokrasia, IDEA itawasilisha mada yake ya sera "Uchaguzi katika hatua ya kuvuka:zingatio la muundo wa uchaguzi baada ya mapinduzi ya Myanmar” ambayo inaeleza maeneo muhimu ya kuzingatia kwa ajili ya uchaguzi wa kweli wa kidemokrasia katika muktadha unaoibukia wa katiba mpya, mfumo mzima wa kisheria wa uchaguzi, chaguo mfumo wa upigaji kurai, usimamizi wa uchaguzi, usajili wa wapigakura, ikiwa ni pamoja na mfumo wa wazi wa haki wa kupiga kura, na utatuzi wa migogoro ya uchaguzi.