Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO lazindua Baraza jipya la vijana

WHO lazindua Baraza jipya la vijana
WHO / Chris Black
WHO lazindua Baraza jipya la vijana

WHO lazindua Baraza jipya la vijana

Afya

Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO limezindua Baraza la vijana lililofanyika kuanzia tarehe 27- 30 Januari 2023 jijini Geneva Uswisi na kuwaleta pamoja viongozi vijana kutoka mashirika 22 ya vijana duniani yanayojishughulisha na masuala ya afya na masuala yasiyo ya afya.

Lengo la baraza hilo ni kuwasikiliza vijana, kupata utaalamu na uzoefu wao katika masuala ya afya kwa umma pamoja na kufanya nao kazi katika kutengeneza harakati za vijana katika afya.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema “Baraza la Vijana ni kipengele kikuu cha dhamira ya WHO ya kushirikiana na vijana, kwa kuunga mkono uongozi wao, kukuza ushirikiano, na kutetea kutambuliwa kwao na kuonekana, kwani sauti zako na maarifa yao yanaweza kuleta mabadiliko ya kweli katika kutimiza maono ya WHO ya Afya kwa Wote.”

Baraza litafanya nini?

Baraza la Vijana litatoa ushauri kuhusu masuala ya afya na maendeleo yanayowahusu vijana, likiwashirikisha kikamilifu Mkurugenzi Mkuu wa WHO pamoja na uongozi wa juu wa WHO.

Baraza hilo pia litatumika kama jukwaa la kubuni na kuingiza mipango mipya, na pia kupanua shughuli zilizopo za ushiriki wa vijana za WHO.

Kupitia Baraza la Vijana, WHO itatayarisha Mkakati wa Ushirikiano wa Vijana katika ngazi zote za shirika.

Nini kimejadiliwa kwenye mkutano?

Wakati wa mkutano wa siku nne, wanachama wa Baraza la Vijana walijadili vipaumbele muhimu na mipango ya kazi ili kuharakisha kuna maendeleo katika upatikanaji wa huduma ya afya kwa wote, magonjwa yasiyo ya kuambukiza, afya ya akili, na vijana kuongoza katika masuala ya afya.

Wahudhuriaji wakati wa kujadili kuhusu mipango madhubuti ya baraza hilo walitangamana na Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Mwenyekiti wa Baraza Kuu la WHO, Dk Kerstin Vesna Petrič, na viongozi wengine wangazi za juu wa WHO.

Matokeo ya mkutano huo

Matokeo kadhaa muhimu ya mkutano ni pamoja na:-

1. kukubaliana juu ya taratibu za kutengeneza fursa za ushirikiano ili ziweze kupatikana kwa vijana kote ulimwenguni kupitia mitandao inayowakilishwa na wanachama wa Baraza la Vijana na kwingineko.

2. kutambua njia za zitakazo wezesha Baraza la Vijana ili kuonyesha kazi zao wakati wa mikutano muhimu ya WHO na matukio ya ushirikiano.

3.Kuchunguza mapungufu katika upatikanaji wa takwimu kuhusu masuala ya usawa wa afya ya vijana na kutambua msaada wa kiufundi wa WHO ambapo wataenda kuripoti mapungufu hayo.

4. Kuandaa pendekezo la kushirikiana na Nchi Wanachama wa WHO Kama hatua ya kwanza. Baraza la Vijana lilitambua fursa za kujumuishwa kwa wajumbe vijana kama sehemu ya wajumbe kutoka Nchi Wanachama na kuandaa mbinu za kuunganisha programu za wajumbe wa vijana kwa msaada kutoka kwa uongozi wa WHO.