Uchumi wa dunia unasuasua huku mazingira ya kifedha yakizidi kuwa magumu:IMF
Shirika la fedha duniani IMF kupitia taarifa yake kuhusu mapato ya serikali na maendeleo ya kifedha iliyotolewa leo limeonya kwamba uchumi wa dunia unazorota wakati huu ambapo mazingira ya kifedha kote duniani yanaendelea kuwa magumu.