Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNDP yatoa wito wa msamaha wa madeni kwa nchi 54

Sudan Kusini imesalia kuwa moja ya nchi masikini duniani
UNMISS
Sudan Kusini imesalia kuwa moja ya nchi masikini duniani

UNDP yatoa wito wa msamaha wa madeni kwa nchi 54

Ukuaji wa Kiuchumi

Nchi 54 ambazo ni makazi ya zaidi ya nusu ya watu maskini zaidi duniani zinahitaji msamaha wa haraka wa madeni limesema Shirika la Umoja wa Mataifa la  Mpango wa Maendeleo UNDP katika jarida lake lililochapishwa leo ambalo inatoa wito kwa nchi tajiri kujitokeza kusaidia.

UNDP imesema bila kuchukuliwa kwa hatua za makusudi, umaskini utaongezeka na uwekezaji unahitajika sana katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kukabiliana na mnepo kutashindikana iwapo msaada hautapatikana.

Jarida hilo lenye jina  Kuepuka ‘Kuchelewa Kidogo’ kwa Msaada wa Madeni ya Kimataifa – linaangazia athari mbaya za namna serikali zinavyoshughulikia mzozo wa hivi karibuni wa kiuchumi, na athari zinazoweza kutokea.

‘Kidonge kidogo’ cha kumeza

Jarida hilo limeeleza kwa nini kufanyia marekebisho kwenye deni hakuwezi kusubiri hadi viwango vya riba vipungue, au kushuka kwa uchumi duniani kutokea.

"Msamaha wa deni ungekuwa kidonge kidogo kwa nchi tajiri kumeza, lakini gharama ya kutochukua hatua ni ya kikatili kwa watu maskini zaidi duniani. Hatuwezi kumudu kurudia makosa ya kutoa unafuu mdogo sana, tumechelewa sana, katika kusimamia mzigo wa madeni ya uchumi unaoendelea," amesema Achim Steiner, Msimamizi wa UNDP.

Nchi 54 zenye matatizo makubwa ya madeni ni pamoja na mataifa 28 kati ya 50 yaliyoathiriwa zaidi na mabadiliko ya tabianchi duniani.

Nchi hizo ingawa ni nyumbani kwa zaidi ya nusu ya watu maskini zaidi duniani, wanawakilisha chini ya asilimia tatu ya uchumi wa dunia.

Haiti ni moja ya nchi masikini zaidi duniani ambako wananchi wake wanaishi kwakutegemea misaada kutoka kweney mashirika ya misaada
IFRC

Mpango wa deni unaowezekana

Jarida hilo limeangazia hatua kadhaa za sera za urekebishaji wa deni, ikibainisha kuwa mpango unaweza kuwa katika upeo wa macho.

Hali ya soko kote ulimwenguni inabadilika haraka. UNDP ilisema hali tete inachochewa na "msukumo wa usawa wa kiuchumi na fedha", pamoja na ukuaji mdogo.

Hivi sasa, karibu nchi 20 zinazoendelea sasa zinalipa zaidi ya asilimia 10 ya viwango vya dhamana za Hazina ya Marekani ili kukopa pesa kwenye masoko ya mitaji.

Wakati huo huo, wamiliki wa dhamana nyingi za uchumi zinazoendelea wanaripoti kuwa wanafanya biashara kwa punguzo kubwa kuanzia kati ya senti 40 hadi 60 kwa dola.

 

Masharti yanavutia mazungumzo

Mpango wa madeni unaweza sasa kuwezekana, UNDP ilisema, kwani masharti haya yanawahimiza wakopeshaji binafsi kujadiliana kuhusu msamaha wa deni chini ya Mfumo wa Pamoja uliofafanuliwa na kundi la nchi za G20, nchi zenye uchumi mkubwa zaidi duniani.

"Wakati dhamana za soko zinazoibuka zinafanya biashara kwa senti 40 kwa dola, wadai wa kibinafsi ghafla wanakuwa wazi zaidi kwa mazungumzo. Kiambatisho kinachokosekana, kwa wakati huu, ni uhakikisho wa kifedha kutoka kwa serikali kuu za wadai ili kufikia makubaliano," George Gray Molina, Mchumi Mwandamizi katika UNDP alisema.

Nchi tajiri zina rasilimali za kumaliza mzozo wa madeni, jarida hilo linasema, kwani kuzorota kwa kasi kwa sehemu kunatokana na sera zao za ndani.

Wiki hii, mawaziri wa fedha wa G20 watakutana Washington, DC, Marekani kabla ya mikutano ya kila mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).

UNDP inaamini kuwa hali ziko tayari kwa wadai na wadeni kuanzisha mazungumzo ya kurekebisha deni chini ya mfumo wa G20.

Jarida hilo linapendekeza njia ya kusonga mbele, inayolenga maeneo muhimu kama vile uchanganuzi wa uhimilivu wa deni, uratibu rasmi wa mdai, ushiriki wa wadai wa kibinafsi, na utumiaji wa vifungu vya deni vinavyotegemea serikali ambavyo vinalenga ustahimilivu wa kiuchumi na kifedha wa siku zijazo.

Ufadhili wa mabadiliko ya tabianchi nao pia unahitajika

Zaidi ya hayo, Mfumo wa pamoja unaweza kuelekeza umakini kwenye urekebishaji wa kina ambao utaruhusu nchi kurudi kwa kasi katika ukuaji, masoko ya fedha na maendeleo endelevu.

UNDP ilisema kuwa urekebishaji mzuri wa madeni ni kipengele kimoja tu muhimu cha kuhakikisha nchi zinazoendelea zina fedha za kutosha kufikia maendeleo.

Vyanzo vipya vya ufadhili vinahitajika haraka, shirika hilo lilisema, kwa uwekezaji katika kukabiliana na hali ya hewa na kupunguza.