Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuna uhusiano baina ya hukumu ya kifo, utesaji na ukatili mwingine: Wataalam UN 

Tukio la hali ya juu kuhusu,hukumu ya kifo.
UN Photo
Tukio la hali ya juu kuhusu,hukumu ya kifo.

Kuna uhusiano baina ya hukumu ya kifo, utesaji na ukatili mwingine: Wataalam UN 

Haki za binadamu

Katika maadhimiosho ya 20 ya siku ya kupinga hukumu ya kifo duniani hii leo, wataalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu utesaji na ukatiuli mwingine , vitendo visivyo vya kibinadamu au vitendo vya udhalilishaji na adhabu Alice Edward, na yule wa kupinga mauaji ya kiholela, Morris Tidball-Binz wametoa taarifa ya pamoja inayotathimini uhusiano baina ya hukumu ya kifo na kupinga kabisa mateso na adhabu nyingine za kikatili, za kinyama au za kudhalilisha.  

Wataalam hao wamesema "Ingawa adhabu ya kifo inaruhusiwa katika mazingira machache sana chini ya sheria za kimataifa, ukweli unabakia kuwa kiutendaji ni vigumu kwa mataifa kutoa adhabu ya kifo wakati ikitimiza wajibu wao wa kuheshimu haki za binadamu za wale waliotiwa hatiani. Kukomeshwa kwa hukumu ya kifo ndiyo njia pekee inayowezekana.” 

Hukumu ya kifo ni utesaji 

Tukio la hukumu ya kifo kwa muda mrefu limejulikana kama aina ya unyanyasaji wa kibinadamu, kama vile kutengwa kwa karibu kwa wale waliopatikana na hatia ya uhalifu wa kifo na mara nyingi huwekwa katika vifungo vya faragha kinyume cha sheria. 

Taarifa yao imeendelea kusema kuwa “Mataifa kadhaa yanaendelea kutoa hukumu ya kifo kwa makosa yasiyo ya ukatili kama vile kukufuru, uzinzi na makosa yanayohusiana na madawa ya kulevya, ambayo hayakidhi kuwa kiwango cha uhalifu mbaya zaidi wa matumizi ya adhabu ya kifo chini ya sheria za kimataifa. Na mwenendo unaoongezeka wa kutoa hukumu ya kifo kwa wale wanaotumia haki yao ya maandamano ya amani ya kisiasa unatia wasiwasi sana.” 

Zaidi ya hayo, wataalam hao wamesema mbinu zinazoongezeka za utekelezaji wa adhabu ya kifo zimegunduliwa kuwa haziendani na wajibu wa kujiepusha na mateso na unyanyasaji, kwa kusababisha maumivu makali na mateso. 

Idadi ya hukumu za kifo inaongezka 

Kwa mujibu wa takwimu za ofisi ya haki za binadamu “Licha ya zaidi ya mataifa 170 kufuta hukumu ya kifo au kupitisha sheri ya kusitishwa, kumeripotiwa ongezeko la asilimia 20 la idadi ya watu walionyongwa mwaka jana.” 

Mataifa ambayo yanabaki na hukumu ya kifo yanahimizwa kujizuia na utekelezaji wa huku hiyo kwa uangalifu hasa kwa watu wenye matatizo ya akili, wanawake wajawazito na watoto, kama inavyotakiwa na vyombo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kifungu cha 6 cha mkataba wa kimataifa wa haki za kiraia na kisiasa (ICCPR). 

Mataifa yote yamealikwa kuzingatia kuidhinisha itifaki ya pili ya hiari kwa ICCPR inayolenga kukomesha hukumu ya kifo.  

“Itifaki hiyo kwa sasa ina watia saini 40 na wanachama kutoka mataifa 90."