Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Mtoto mwenye umri wa miaka 11 akijipatia ahueni ya joto kali kwa kucheza kwenye chemchem ya maji huko  Uzbekhstan
UNICEF/Pirozzi

Watoto milioni 559 duniani kote wanataabika na joto kali kwa sasa, idadi itaongeza na kufikia zaidi ya bilioni 2 mwaka 2050.

Kuelekea mkutano wa 27 wa nchi wanachama wa mkataba wa kimataifa wa mabadiliko ya tabianchi, COP27utakaofanyika nchini Misri barani Afrika, shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya watoto UNICEF wametoa ripoti ya kuonesha athari za mabadiliko ya tabianchi kwa watoto katika kipindi cha kuanzia sasa mpaka mwaka 2050.

 Katibu Mkuu António Guterres (kushoto) amekutana na Nguyen Phu Trong, Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti, huko Hanoi, Viet Nam.
UN Photo/Minh Hoang

Guterres aikumbusha Viet Nam umuhimu wa mifumo ya tahadhari ya mapema

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo ameendelea na ziara yake nchini Viet Nam ambapo ametembelea kituo cha hali ya hewa na nguvu za maji cha nchi hiyo na kuwakumbusha viongozi wa kituo hicho kuhusu umuhimu wa kujitayarisha kwa maafa yanayoweza kutokea na kusema lengo ni kuwa na mifumo ya tahadhari ya mapema katika nchi zote duniani ndani ya miaka mitano.