Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kijiji cha kwanza nchini India kinachotumia nishati ya jua kinakuza nishati ya kijani, endelevu na inayojitegemea

Gadvi Kailashben, mjane mwenye umri wa miaka 42, anaishi Modhera, kijiji cha kwanza nchini India kinachotumia nishati ya jua. Alisema paneli za jua zilizowekwa kwenye nyumba yake zimetoa unafuu unaohitajika kutokana na gharama za nyumbani.
UN News
Gadvi Kailashben, mjane mwenye umri wa miaka 42, anaishi Modhera, kijiji cha kwanza nchini India kinachotumia nishati ya jua. Alisema paneli za jua zilizowekwa kwenye nyumba yake zimetoa unafuu unaohitajika kutokana na gharama za nyumbani.

Kijiji cha kwanza nchini India kinachotumia nishati ya jua kinakuza nishati ya kijani, endelevu na inayojitegemea

Tabianchi na mazingira

Katika ziara yake ya siku mbili nchini India, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres alitembelea eneo la mradi wa mfano katika jimbo la Gujarat, lililoteuliwa kuwa kijiji cha kwanza cha nishati ya jua nchini humo.

Akiwa kijijini hapo aliwapongeza wanakijiji kwa kuhamia kwenye nishati mbadala, ambayo alisema sio tu kunabadilisha maisha ya jamii, lakini pia wanasaidia kupambana na mabadiliko ya tabianchi.

Gadvi Kailashben, mjane mwenye umri wa miaka 42, anaishi Modhera, eneo maarufu kama nyumbani kwa Jumba la jua “Sun Temple” jumba hili la karne nyingi na sasa ni Kijiji cha kwanza nchini India kinachotumia nishati ya jua.

Anapata kipato kidogo kutokana na kilimo ambacho anakitumia kutunza familia yake. Serikali imeweka paneli za sola kwenye nyumba yake ambayo imempa unafuu unaohitajika kutokana na gharama za nyumbani.

"Hapo awali, wakati nishati ya jua haikuwepo, ilibidi nilipe kiasi kikubwa cha bili ya umeme - karibu rupia 2,000. Hata hivyo, pamoja na ufungaji wa sola, bili yangu ya umeme sasa ni sifuri. Kila kitu kutoka kwenye jokofu hadi mashine ya kuosha sasa kinatumia jua ndani ya nyumba yangu. Silipi hata bili ya umeme ya rupia 1 sasa,” amesema Bi Kailashben.

"Pesa za ziada sasa zimehifadhiwa kwenye akaunti yangu. Ninatumia pesa hizo kwa matumizi ya kila siku ya nyumba, na kwa elimu ya watoto wangu,” aliongeza.

Huku bili ya umeme ikipunguzwa, Ashaben sio tu kwamba anaokoa pesa alizotumia kwa umeme, lakini ziada ya umeme inayozalishwa inauzwa kwenye gridi ya taifa na anapata pesa kama malipo.
UN News
Huku bili ya umeme ikipunguzwa, Ashaben sio tu kwamba anaokoa pesa alizotumia kwa umeme, lakini ziada ya umeme inayozalishwa inauzwa kwenye gridi ya taifa na anapata pesa kama malipo.

Nishati mbadala kama chanzo cha mapato

Kugeukia chanzo safi cha nishati mbadala sio tu kumewawezesha wanakijiji kuendesha vifaa vingi vya umeme vya nyumbani ili kufanya maisha kuwa ya starehe, bila kuwa na wasiwasi kuhusu bili ya umeme. Pia inakuwa chanzo cha mapato kwao.

Ashaben Mahendrabhai, mwenye umri wa miaka 38, anaishi na mumewe na watoto wawili. "Tunafanya kazi katika shamba letu na tulikuwa tunalipa bili kubwa ya umeme kwa kilimo. Tangu kuwekwa kwenye sola katika kijiji chetu, sasa tunaokoa umeme mwingi. Hapo awali bili yetu ya umeme ilikuwa ikija karibu rupia 2,000. Sasa ni katika hasi, "alisema.

Huku bili ya umeme ikipunguzwa, Ashaben sio tu kwamba anaokoa pesa alizotumia kwa umeme, lakini ziada ya umeme inayozalishwa inauzwa kwenye gridi ya taifa na anapata pesa kama malipo.

"Wakati timu ya mradi ilipotujia na wazo la sola, hatukuelewa dhana hiyo, kwa hivyo tulikataa kuiweka. Hatukuwa wasomi kuelewa nishati ya jua ilikuwa nini na tulikuwa na ufahamu mdogo juu yake. Lakini polepole, timu ilitufanya kuelewa dhana na faida za sola, jinsi tutakavyookoa umeme na pesa, ndipo tukavutiwa nayo, "alisema.

Pingalsinh Karsanbhai (kulia) anahisi kuwa mradi hautoi tu uhuru kutoka kwa bili za umeme, lakini "uhifadhi huu ni kama pensheni kwa uzee wetu."
UN News
Pingalsinh Karsanbhai (kulia) anahisi kuwa mradi hautoi tu uhuru kutoka kwa bili za umeme, lakini "uhifadhi huu ni kama pensheni kwa uzee wetu."

Wakulima wa eneo hilo Pingalsinh Karsanbhai Gadhvi na Surajben Gadhvi, ambao wamefunga ndoa hivi karibuni, walipata paa za jua zilizowekwa kwenye nyumba yao miezi sita iliyopita.

Pingalsinh Karsanbhai anahisi kuwa mradi huu haujawapa tu uhuru kutoka kwenye bili za umeme, lakini akiba itawaweka katika nafasi nzuri katika uzee wao.

“Hapo awali tulikuwa tunapata bili ya umeme ya rupia 3,000 na baada ya sola sasa hatulipi kitu chochote yanu ni sifuri. Sasa tunaokoa hizo rupia 3,000 kila mwezi,” alisema.

Wakazi wa kijiji cha kwanza cha miale ya jua nchini India wakitangamana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wakati wa ziara yake.
UN News
Wakazi wa kijiji cha kwanza cha miale ya jua nchini India wakitangamana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wakati wa ziara yake.

Alifafanua zaidi kwamba “uhifadhi huu wa fedha ni kama pensheni kwa uzee wetu. Tumefurahi sana kuhusu hilo.”

Mkewe Surajben alikuwa akitabasamu na alikuwa na furaha sana kwa kijiji chake kupendekezwa kabla ya vijiji vingine.

"Ikiwa sola hii itawekwa nchini kwetu kote itakuwa na faida kubwa. Inahisi kama Mungu wa Jua anatupa nishati kupitia mwanga wake. Faida hii ambayo kijiji chetu cha Modera kimepata, inapaswa kufikia nchi nzima,” alisema.

Akishirikiana na wanakijiji wa Modhera wakati wa ziara yake, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres alipongeza juhudi za Serikali na wakazi.

“Hapa ambapo Hekalu la Jua lilijengwa miaka 1,000 iliyopita, kuna Hekalu jipya la Jua.Linategemea nishati ya jua. Na ukweli kwamba nishati ya jua inabadilisha maisha ya watu wa kijiji hiki, na kuifanya kuwa na afya zaidi, kuwapa ustawi zaidi, lakini wakati huo huo, kuchangia kuokoa sayari yetu kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa ambayo bado yanazunguka bila kudhibitiwa.

Hekalu la Modhera Sun huko Gujarat, India, sasa linaendesha onyesho la mwanga wa 3D kuhusu nishati ya jua.
UN News
Hekalu la Modhera Sun huko Gujarat, India, sasa linaendesha onyesho la mwanga wa 3D kuhusu nishati ya jua.

Kuvutiwa kutoka kwa Mungu wa Jua

Nyumbani kwa Hekalu la Jua la Gujarat, kijiji cha Modera ni takriban kilomita 97 kutoka mji wa Ahmedabad katika wilaya ya Mehsana ya Gujarat.

Kwa maono ya kuwezesha Hekalu la Jua na kijiji kizima kupitia Mungu wa Jua (nishati ya jua), mradi huu ni wa kwanza wa aina yake, ambapo wakazi wa vijijini wanatarajiwa kujitegemea kupitia nishati ya kijani.

"Wazo la mradi huu ni kwamba kwa kuwa hekalu la Modera ni Hekalu la Mungu wa Jua, hivyo nishati yote ya mji huu na jumuiya inapaswa kutoka kwa nishati ya jua," alisema Mamta Verma, Katibu Mkuu, Nishati na Petrochemicals katika Serikali ya Kigujarat.

Hekalu la Mungu au kwa kiingereza The Sun Temple sasa inaendesha onyesho la mwanga wa 3D kabisa kwenye nishati ya jua, majengo yake yanatumia nishati ya jua na eneo la maegesho pia linajivunia vituo vya kuchaji magari ya umeme.

Vituo vya kuchaji vya magari yanayotumia nishati ya jua katika Jumba la Sun Temple huko Modhere, India.
UN News
Vituo vya kuchaji vya magari yanayotumia nishati ya jua katika Jumba la Sun Temple huko Modhere, India.

Hifadhi ya nishati mbadala

Ikiwa na safu kubwa ya paneli za jua kwenye paa za nyumba, kwenye shule za Serikali, vituo vya mabasi, majengo ya matumizi, maegesho ya magari na hata majengo ya Jumba la Jua, (Sun Temple), Modhere inanufaika na mtambo wa kuzalisha umeme wa megawati sita uliowekwa katika kijiji cha Sujjanpura kilicho karibu.

Kwa matumizi ya kijiji  ni megawati moja hadi mbili, ziada huongezwa kwenye gridi ya usambazaji.

Shule za serikali, vituo vya mabasi na majengo ya matumizi katika kijiji cha Modera huko Gujarat, India, sasa yanatumia nishati ya jua.
UN News
Shule za serikali, vituo vya mabasi na majengo ya matumizi katika kijiji cha Modera huko Gujarat, India, sasa yanatumia nishati ya jua.

"Kuna sehemu tatu kuu za mradi huu wote. Moja ni mradi wetu wa megawati 6 zilizowekwa ardhini. Ya pili ni mfumo wa kuhifadhi betri wa megawati 15 na ya tatu ni ya paa ya kilowati moja iliyowekwa kwenye nyumba 1,300,” Afisa Mkuu wa Miradi wa Kampuni ya Gujarat Power Corporation Limited (GPCL), Rajendra Mistry, alieleza.

"Kati ya paa 1,000 tulizotoa katika kijiji hicho, umeme unaotoka kwanza unatumiwa na wananchi wa kijiji hicho, na umeme unaozidi unatolewa kwenye gridi ya taifa."

Ukifadhiliwa na Serikali ya India na Serikali ya eneo la Gujarat, makadirio ya gharama ya mradi mzima ni dola milioni 9.7. Kinachoitofautisha ni ukweli kwamba Modhera pia ni kijiji cha kwanza kuwa jenereta ya nishati mbadala.

Paneli za miale ya jua kwenye paa za nyumba huko Modera, iliyoko katika jimbo la Gujarat, India.
UN News
Paneli za miale ya jua kwenye paa za nyumba huko Modera, iliyoko katika jimbo la Gujarat, India.

"Hiki ni kijiji cha kwanza nchini India ambapo hata wakati wa usiku, nishati inayotumiwa na wanakijiji inatoka kwa sehemu ya jua. Huo ndio utaalam wa mradi huu, "alisema Vikalp Bharwaj, Mkurugenzi Mkuu wa Gujarat Power Corporation Limited.

Maono ya siku zijazo

Mradi huu wa maonesho unatarajiwa kutoa mafunzo ya kutatua vikwazo vinavyohusiana na nishati mbadala. Iwapo mradi utathibitika kuwa mzuri kiuchumi, mpango ni kuuiga katika maeneo mengine ya mashambani huko Gujarat.

Alisema Bharwaj: “Mradi wa aina hii unafanya kazi kama mradi wa maonesho kwa vijiji na miji mingine nchini India. Na vile vile, vijiji na miji mingine inaweza kupitisha mtindo huu ili kujitegemea, kujitosheleza katika mahitaji ya nishati.

Mkazi wa Modera Ashaben Mahendrabhai alitoa muhtasari wa manufaa hayo.

"Ningehimiza vijiji vingine pia kuweka nishati ya jua kwa kuwa ina manufaa katika nyanja zote, kutoka kuokoa fedha hadi kuokoa umeme," alisema.

Modera inanufaika kutoka kwa kiwanda cha nguvu cha Megawati 6 kilichowekwa katika kijiji cha karibu cha Sujjanpura.
UN News
Modera inanufaika kutoka kwa kiwanda cha nguvu cha Megawati 6 kilichowekwa katika kijiji cha karibu cha Sujjanpura.

UWEKEZAJI KWENYE NISHATI YA JUA

  • Zaidi ya kaya 1,300 zina Mifumo ya Nishati ya Jua ya paa ya KW 1 kwenye majengo ya Makazi. Uwezo wa 316 KW kwenye mifumo ya paa kwenye majengo mbalimbali ya serikali katika vijiji vya Modera, Samlanpura na Sujjanpura.
  • Kiwanda Kinachounganishwa kwenye Gridi ya MW 6 cha Umeme Kilichowekwa kwenye Sola ya PV huko Sujjanpura
  • MWh 15, MW 6, Mfumo wa Kuhifadhi Nishati ya Betri (BESS) huko Sujjanpura.
  • Modhere hutumia 1Mw pekee, na zinazosalia zinapelekwa kwenye gridi ya taifa.
  • Ufungaji wa Meta za Nishati Mahiri (zaidi ya 1700) katika kiwango cha watumiaji wa umeme.
  • Hekalu la Jua linaloendeshwa kikamilifu na jua huendesha Onyesho la Mwanga la makadirio ya 3D kwenye nishati mbadala.
  • Kumewekwa taa mahiri za barabarani kulingana na vitambuzi, karibu na Hekalu la Jua.
  • Miundombinu ya Maegesho ya Jua ya 50 KWh yenye Hifadhi ya Betri ya kWh 150 yenye Vituo vya Kuchaji Umeme kwenye Hekalu la Modhera Sun.