Azimio lapitishwa kuchochea kasi ya kusaidia wakimbizi wa CAR
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR na serikali za mataifa ya Afrika ya Kati wamepitisha azimio jipya linalotoa wito wa kuchukuliwa hatua zaidi kusaidia wakimbizi zaidi ya milioni 1.4 waliofurushwa kutokana na mzozo wa Jamhuri ya Afrika ya Kati.